Na Lucy Lyatuu
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania TTCL limefanya maboresho makubwa kwa watumiaji wa simu za mkononi kwa kufanya watanzania wote Bara na Zanzibar kupata huduma mahali popote walipo bila vikwazo vyovyote.
Maboresho hayo ni Pamoja na ukomo wa matumizi ya vifurushi pamoja na kiwango cha fedha ikiwa ni kuwapa fursa ya kuwasiliana kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Vedastus Wambura amesema Mawasiliano ni chachu kubwa ya biashara mtandaoni ambayo inahitaji kutumia huduma hiyo kwa gharama nafuu pamoja na kupata vifurushi ambavyo vitatumika mpaka mwisho badala ya kupewa muda maalum wa matumizi.
Amesema katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma hizo TTCL imekuja na kampeni ya Walete Nyumbani mambo ni moto ikilenga zaidi kuwaleta watanzania kutumia hudum za TTCL katika maeneo makuu matatu.
Kampeni hiyo inaongozwa na Balozi Clayton Chipando maarufu kama babalevo.
Ameyataja maeneo yatakayoguswa na kampeni hiyo kuwa ni huduma za data, kurahisisha na.kuboresha huduma za sauti na kupata muda wa maongezi bila kuwa na kikwazo cha muda wa matumizi na pesa.
Amesema Mawasiliano ni chachu kwenye biashara na kwamba kampeni hiyo umekuja kuondoa vikwazo mbalimbali vya vifurusgi vya Mawasiliano.
Amesema kupitia kampeni ya Walete itakuwa na kifurushi Cha bufee Tena kitakachoqezesha mtu yoyote mwenye kifurushi chochote kutengeneza kifurushi anachotaka.
” Hapa ina maana kuwa iwapo mtu ana shilingi mbili kwenye simu yake anaweza kupata data kulingana na kiwango alicho nacho kwenye simu,’ amesema na kuongeza pia kitaondoa kikwazo Cha kwamba lazima kuwa na kiwango Fulani Kwa simu ndipo uweze kujiunga.
Amesema eneo lingine litakaloguswa na kampeni ni kuwa na kifurushi Cha Jiachie extra ambacho ni Cha sauti na ujumbe mfupi pekee.
” Ukishajiunga mpaka fedha yako kwenye vifurusgi itakapokwisha sio kwamba baada ya saa fulani kinakata,” amesema.
Kadhalika amesema eneo lingine ni kuwepo kwa kifurushi Cha T Connect Plus kinachowahusu watumia data pekee.
Amesema kifurushi hicho ni Kwa ajili ya wenye simu janja zenye kutumia data ambapo itasaidia Watanzania kuondoka kwenye changamoto ya namna ya kumaliza fedha za kifurushi alichojiunga nacho lakini pia kupata huduma Bora zaidi.