Na Lucy Ngowi
CHAMA cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) kimezindua kampeni ya Afya na Usalama Mahala Pa Kazi itakayowafikia wafanyakazi wao katika maeneo yanayofika reli ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
TRAWU imezindua kampeni hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa Afya na Usalama Mahala pa Kazi (OSHA) pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ( WCF),
Naibu Katibu Mkuu wa TRAWU, Edo Makatta amesema kwamba wameshazindua kampeni hiyo upande wa TAZARA ambapo semina ya kwanza imefanyika mkoani Dar es Salaam mwezi huu, ambapo OSHA na WCF ndio wwaliotoa mafunzo hayo.
Amesema kampeni hiyo ni chachu ya kuwaunganisha wafanyakazi kuwa na mshikamano na umoja katika kusimamia ki na masslahi y wafanyakazi.
“Hii ni kampeni maalum na endelevu ambapo tunataraji wafanyakazi waliopo Mashirika ya Reli nchini yaani TAZARA na TRC na nilisema TRC namaanisha ndani wamo SGR. Hivyo kuridhia kwa OSHA na WCF kumetusaidia sana kupunguza gharama za kulipa wawezeshaji ambazo zimebebwa na taasisi husika. Tunatumia nafasi hii kuzushukuru Taasisi hizi kuridhia kufanya kazi na TRAWU. Huu ni mwanzo mzuri na tunaamini tutafanyia nao kazi maeneo mengi.
“‘Semina hizi zitawafungua wafanyakazi juu ya haki zao za kimsingi kuhusu nini OSHA wanawajibika kwa wafanyakazi na nini WCF unahudumia wafanyakazi. Mambo ni mengi wameanza kuelimishwa juu ya Haki zao na ni Imani Elimu hii itasambaa,” amesema.