MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TIRA Yasisitiza Umuhimu wa Bima katika Kulinda Uchumi wa Taifa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TIRA Yasisitiza Umuhimu wa Bima katika Kulinda Uchumi wa Taifa
Habari

TIRA Yasisitiza Umuhimu wa Bima katika Kulinda Uchumi wa Taifa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
TANGA: bAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imesisitiza kuwa bima ni nyenzo muhimu ya kulinda maisha ya wananchi na uchumi wa taifa, na si jambo la hiari kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidhani.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea mkoani Tanga kuanzia Januari 19 haLupilyamwaka huu 2026, Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini, Dkt. Emmanuel Lupilya, amesema bima ina mchango mkubwa katika kulinda shughuli za kilimo,
Biashara na uzalishaji, pamoja na kupunguza athari za majanga kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa baada ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dadi Kolimba, kutembelea banda la TIRA katika maadhimisho hayo.
Dkt. Lupilya amesema TIRA haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya makampuni ya bima yatakayokiuka miongozo, sheria na taratibu zilizowekwa, akisisitiza kuwa ukiukwaji wa sheria hizo unakwamisha ukuaji wa sekta ya bima na maendeleo ya uchumi wa taifa.
Ameeleza kuwa mamlaka hiyo, kwa kushirikiana na makampuni ya bima, inaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza uelewa wa masuala ya bima, akibainisha kuwa ukosefu wa elimu hiyo hulazimisha serikali kubeba mzigo mkubwa wa kifedha unaotokana na majanga, umaskini na mdororo wa uchumi.
“Endapo taifa halitaelimishwa kuhusu umuhimu wa bima, serikali italazimika kugharamia athari za majanga, umaskini na kushuka kwa shughuli za uzalishaji, hali inayoliletea taifa mzigo mkubwa wa kiuchumi,” amesema.
Ameongeza kuwa juhudi za TIRA na makampuni ya bima katika kutoa elimu kwa umma ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha ukuaji wa pato la taifa na kuimarisha ustawi wa wananchi.
Sambamba na hilo, amezitaka kampuni za bima kuwa wabunifu katika kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji halisi ya wananchi, badala ya kuangazia zaidi maslahi ya makampuni yenyewe.

You Might Also Like

Mwalim: Ardhi Yetu ni Ufunguo wa Uhuru wa Kiuchumi

Tanzania Yapiga Hatua Kwenye Elimu ya Kidijitali Kupitia Ushirikiano na China

Maabara Za Sayansi Zachochea Hamasa Kitaaluma

Tani 27, 550  za ufuta zenye thamani ya bilioni 80 zimeuzwa

Wizara  Ya Maliasili Na Utalii Ilivyotamba Na Historia Ya Faru John Na Faru Fausta Mbele Ya Kamati Ya Bunge

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wiki ya Huduma za Fedha: SELF Yafungua Fursa za Kiuchumi kwa Wananchi Tanga
Next Article Uwekezaji wa TIB Wachangia Kuongezeka kwa Ajira
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mavunde: Makaa ya Mawe Ni Injini ya Maendeleo ya Viwanda
Habari March 30, 2026
Programu Mpya ya TPHPA Yalenga Usalama wa Mazao Sokoni
Habari March 30, 2026
CHAKUHAWATA Yaimarisha Ulinzi wa Haki za Walimu, Yafikia Wanachama 49,750
Habari March 29, 2026
Upungufu wa Wataalamu wa Ustawi wa Jamii Wachangia Changamoto Kwenye Huduma za Jamii
Habari March 28, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?