Na Lucy Ngowi
DODOMA: KAMPUNI ya Simu za mkononi, Mtandao wa Tigo umewakaribisha wakulima, wafugaji na Wavuvi kutumia mtandao huo wenye kasi kubwa kwa ajili ya kuangalia na kutafuta masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kati, Said Iddy amesema hayo katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma.
Amesema lengo la kuwakaribisha wakulima hao kutumia mtandao huo, ni kutokana na maboresho yaliyofanyika na kuwa wenye kasi unaoongoza hapa nchini kwa lengo la kuwasaidia wateja wake kufanya shughuli zao za kilimo, ufugaji na uvuvi kirahisi.
Pia amesema katika kuhakikisha wateja wao ambao ni wakulima, wafugaji na wavuvi wanapata mawasiliano kwa urahisi, Tigo imewaletea bidhaa mpya sokoni ya simu janja za bei nafuu.
Lengo la simu hizo ni kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi hata wenye kipato cha chini kumiliki simu janja na kufanya shughuli zao kimtandao.
Amesema kupitia mtandao wa tigo ulioboreshwa ,wakulima,wafugaji na wavuvi wanakwenda kupata taarifa za masoko ya bidhaa zao na bidhaa nyingine wanazohitaji ili kuboresha shughuli zao.
Amewaasa wananchi,wakulima,wafugaji na wavuvi kufika kwenye banda la Tigo ili wakajipatie bidhaa za mtandao huo wenye kasi ikkwemo simu janja aina ya ZTE A34 inayopatikana kwa mkopo wa kianzio cha shilingi 35,000.
Mkazi wa Chamwino Dodoma, David Mazuguni aliyefika katika banda la Tigo, ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kuweza kumiliki simu janja.