Na Mwandishi Wetu, Pemba
ZANZIBAR: WAZIRI wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamata Shaame Khamis ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), kwa kuwa na teknolojia za kilimo zinazo mwongezea mkulima tija.
Khamis ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la TARI katika Maonesho ya siku ya chakula Duniani yanayofanyika viwanja vya Chamanangwe Kisiwani Pemba.
Maonesho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo, ‘Haki ya Chakula kwa Wote kwa Maisha bora ya Sasa na yajayo’.
Maonesho hayo yanafunguliwa rasmi leo Oktoba 10, 2024, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla.