MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Petroli Afrika
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Petroli Afrika
Habari

Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Petroli Afrika

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Lyatuu

TANZANIA  itakuwa mwenyeji wa mkutano na maonesho ya 11 ya Petroli ya Afrika Mashariki (11TH East African Petroleum Conference and Exhibition – EAPCE’25), unaotarajiwa kufanyika Machi 5 hadi 7, 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)  Dar es Salaam.

Kauli mbiu ya  Mkutano huo, ni “Kufungua Fursa za Uwekezaji katika Nishati, Mchango wa Rasilimali za Mafuta katika Kupata Nishati ya Uhakika kwa Maendeleo Endelevu ya Afrika Mashariki,”.

Mkutano huo utafunguliwa rasmi na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ukitanguliwa na semina kuhusu masuala ya nishati safi ikiwemo nishati safi ya kupikia na matumizi ya gesi kwenye magari (CNG) itakayofanyika Machi 4, 2025.

Mkutano wa EAPCE’25 utawaleta pamoja washiriki zaidi ya 1000, wakiwemo watunga sera, viongozi wa Serikali kutoka nchi mbalimbali ikiwemo nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wawekezaji wa kimataifa na wa ndani.

Akizungumza na vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati  Felchesmi Mramba amesema Mkutano huo utatoa nafasi ya kujadili mchango wa rasilimali za mafuta na gesi asilia katika mchanganyiko wa nishati kwa maendeleo endelevu ya Afrika Mashariki.

Pia washiriki watajadili fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya mafuta na gesi Afrika Mashariki.

Aidha, Mramba ameeleza kuwa mada mbalimbali kutoka kwa wataalam na wabobezi katika sekta ya mafuta na gesi zitatolewa zikiwemo utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi katika nchi za Afrika Mashariki.

Amesema mada nyingine ni fursa za uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa mafuta na gesi, dhana ya kuelekea nishati safi, masuala ya mazingira, miundo ya kisera, kisheria na kiudhibiti katika mafuta na gesi na kadhalika.

Vilevile, mkutano utahusisha maonesho ya bidhaa na huduma kutoka kampuni mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa mafuta na gesi asilia.

Aidha,Mramba ameeleza kuwa Mkutano wa EAPCE’25 unafanyika katika wakati muhimu baada ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kujadilia masuala ya nishati.

Katika mkutano wa Mission 300 nchi za Afrika zilikubaliana kuweka Mpango Mahususi wa Taifa wa Nishati kwa kipindi cha miaka mitano 2025-2030.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kikanda ya maandalizi ya EAPCE’25 ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio aliongeza kuwa Mkutano huu unahusisha pia ziara za kitaaluma katika maeneo ya kijiolojia katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuwapa washiriki mtazamo wa vitendo kuhusu sekta.

 

You Might Also Like

VETA Yatembelea Kiwanda Cha Kutengeneza Nyumba Bila Kutumia Tofali

NBS: Utumiaji Wa Takwimu Nyenzo Muhimu Kwa Mama Lishe

Mrithi wa Kinana Kupatikana Mkutano Mkuu wa CCM

TRA Kupambana Na Wakwepa Kodi Kupitia Bandari Bubu

Chanzo Cha Bunge Kuridhia Hoja Ya Wanaojifungua Njiti, Kilianzia Hapa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wananchi Kutembea Mwendo Mrefu Kutokana Na Upungufu Wa Majengo
Next Article Ushiriki Wa Wanawake, Wasichana Katika Sayansi Ni Mdogo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?