Na Danson Kaijage
DODOMA: MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent amesema kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali Awamu ya Sita, Tanzania imejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 128.
Laurenti amesema hayo alipotoa taarifa ya akitoa taarifa ya mafanikio ya mamlaka hiyo kwa kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema kuwepo kwa utoshelevu wa chakula nchini unatokana na matumizi sahihi ya mbolea yenye ubora inayozalishwa nchini na inayotoka nje ya nchi.
Pia amesema kwa sasa matumizi ya mbolea ya ruzuku inapatikana kwa wakati na kwa bei inayofahamika kwa unafuu wa mkulima ambaye amejisajili.
Akizungumzia mafanikio kwa wakulima ambao wamesajiliwa amesema ni wakulima milioni 4.8 japo wakulima wengi wanahitajika kuendelea kujisajili ili waweze kutambuliwa zaidi kwa lengo la kupatiwa huduma.
Akizungumzia mbolea ya ndani amesema kuwa kwa sasa matumizi ya mbolea ya ndani ni tani laki 1.58 tofauti na miaka ya nyuma ambapo matumizi ya mbolea ya ndani ilikuwa tani 41.
Akizungumzia madeni kwa wasambazaji wa mbolea ya ruzuku amesema kuwa mpaka sasa Serikali imefaniliwa kulipa madeni kwa asilimia 65 ya madeni yote.