Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 19

TALGWU Kufanya Uchaguzi Wa Viongozi Septemba 17

Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Taifa Septemba 17 na 18, mwaka huu 2026, jijini Dodoma, kwa kuzingatia Ibara ya 55.1 ya Katiba ya chama hiyo ya mwaka 2026.
Akitoa taarifa kuhusu mkutano huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TALGWU na Mratibu wa Uchaguzi wa 2026, Shani Kibwasali, amesema utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper, Dodoma.
Amesema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu.
Kwa mujibu wa Kibwasali, mkutano huo utafuatiwa na Baraza Kuu la Taifa litakalofanyika Septemba 19, mwaka huu.
Amesema miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika Mkutano Mkuu ni kupitia taarifa ya utekelezaji wa kazi za chama kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka 2021 hadi 2026.
Aidha, amesema mkutano huo utafanya uchaguzi wa viongozi watakaokiongoza chama kwa kipindi cha mwaka 2026 hadi 2031. Kwa sasa, Mwenyekiti wa TALGWU ni Tumaini Nyamhokya.
Kibwasali amewahamasisha wanachama wa chama hicho kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi huo.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.