MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Simbachawene: Simu za mkononi zinaondoa umakini kwa watumishi wa umma
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Simbachawene: Simu za mkononi zinaondoa umakini kwa watumishi wa umma
Habari

Simbachawene: Simu za mkononi zinaondoa umakini kwa watumishi wa umma

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Simbachawene: Simu za mkononi zinaondoa umakini kwa watumishi wa umma
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema watumishi wengi wa umma wamepoteza umakini kutokana na kushika simu za mkononi ambazo zinawafanya wasahau majukumu yao kwa muda husika.
Simbachawene amesema hayo wakati akifunga semina ya Waajiri na Viongozi wa Matawi ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania ( TUGHE).
“Tunaenda nchi za wenzetu tunaona hawaingii na simu za mkononi ofisini, simu zinawekwa akitoka ndio anachukua na kufanya mawasiliano.
“Sisi watanzania matumizi ya simu yanatumika sivyo ofisini. Makundi yenyewe ni mengi. Kuna kundi la vikoba, la familia, ulilomaliza nao chuo, makundi chungu nzima. Kwa hali hii utahudumia watu saa ngapi?,” amehoji.
Anasema wapo watumishi wanaojitetea ni wafanyakazi wa kazi za ofisini, lakini na muuguzi naye ana makundi amemwekea mgonjwa drip, muuguzi huyo anaendelea kuchati.
Amesema likiwekwa katazo la matumizi ya simu za mkonono ofisini, mgogoro utakuwa ni mkubwa.
“Kama kuna kitu kinachoharibu afya zeru, ukishagusa simu ukitaka kulala usingizi unakata. Tumeathirika na simu, umakini wa kazi unapotea ukishika simu,”amesema.
Amesema watumishi wa umma wasipojikita kufanya kazi kwa bidii, kwa umakini nchi haitasonga mbele.
Kwa upande mwingine amesema watumishi wakitambua wao ni kioo cha jamii ni lazima wavae mavazi yanayokubalika kwa mujibu wa sheria.
Amesema isipowekwa sheria kali za watumishi wa umma,itakuwa kama maeneo mengine duniani.
“Watumishi wa umma baadhi yetu wanavaa vibaya hawajali kanuni za uvaaji. Tukumbuke sisi ni kioo cha jamii lazima uvae vazi linalokubalika kwa mujibu wa sheria.
“Nitamwelekeza Katibu Mkuu kutoa waraka maalum juu ya mavazi ya utumishi wa umma. Kwani huwezi mtumishi wa umma ukaacha bega wazi,” amesema.
Naye Katibu Mkuu Tughe, Hery Mkunda amesema lengo la semina ni kutoa uelewa wa pamoja kati ya waajiri na wafanyakazi sehemu za kazi.
Amesema hilo llitaboresha na kuondoa changamoto.

You Might Also Like

Makamu Mkuu OUT: Elimu ya Masafa Yahitaji Nidhamu ya Hali ya Juu

VETA Mara Wabuni Mtambo Wa Kuchakata Maji Kwa Samaki Wanaofugwa

Tanzania Na Italy Wasaini Makubaliano Kuongeza Ubora Mafunzo Ya Ukarimu

ALAT Kujadili Ripoti Ya CAG

CMSA Yatoa Elimu ya Uwekezaji kwa Wananchi na Wakulima Nanenane

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ujenzi Miundombinu ya Kuongeza Udahili kipaumbele Cha Serikali
Next Article Tanzania yajipanga kutumia nishati ya nyuklia kuzalisha umeme
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

BRELA Kuleta Mradi Wenye Suluhu Kwa Wakulima Na Wafugaji
Habari June 18, 2026
Ridhiwani Aipongeza EWURA kwa Utoaji wa Huduma kwa Wananchi
Habari June 17, 2026
VETA Yazalisha Bidhaa 825, Zinauzwa Ndani Na Nje Ya Nchi
Habari June 17, 2026
 Mfumo Wa REA  Wa Digital Platform  Wapongezwa Na Waziri Kikwete
Habari June 17, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?