Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 3

SIDO jengeni viwanda 20 Kila mkoa-Jafo

Na Lucy Lyatuu
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo ameliagiza Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO) kuandaaa mpango  utakaowezesha ujenzi wa Viwanda vidogo  20 Kwa Kila mkoa Kwa kuwa ,jambo hilo litasaidia kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira nchini.
Amesema lengo la mpango huo ni kuongeza thamani katika Viwanda na mpango huo uwe na matarajio ya kuzinduliwa kati ya  2025 hadi 2030 Ili kujibu matatizo ya wananchi.
Waziri Dkt. Selemani Jafo amesema hayo Dar es salaam alipotembelea Shirika la SIDO Kwa ajili ya kujitambulisha na kusalimia.
Amesema  katika kupambana na tatizo la ajira nchini, huku vijana wengi wakihitimu masomo yao ni muhimu kwa Shirika Hilo kuhakikisha linawezesha  ujenzi wa viwanda mbalimbali katika  Kila mkoa jambo litakalopunguza tatizo la ajira nchini
“Kila mwaka vijana  zaidi ya 64,000 huhitimu kozi mbalimbali na serikali haiwezi kuajiri wote na eneo  kubwa linalotegemewa ni viwanda na Biashara,” amesema na kulitaka Shirika Hilo kupanga mpango wa miaka sita kuanzia 2025-2030 Ili kuwa na viwanda nchini.
Kadhalika amesema chini ya mpango huo,  kila mwaka na Kila mkoa kuhakikisha viwanda vitatu vyenye Hadhi vinajengwa  na ujenzi wa viwanda  vya kati vipatavyo vitano.
Amesema mpango huo wa ujenzi wa viwanda utasaidia ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi.
Waziri Jafo amesema  pamoja na mpango  huo, Kila mkoa uwe na kongani ya kibiashara lengo likiwa ni Kila mkoa kushindana kibiashara.
‘ Katika hili la kongani, watu waangalie mahitaji na  fursa ,zilizopo kwenye maeneo yao,” amesema Jafo na kuongeza kuwa kipindi hiki ni Kwa ajili ya kufungua mikanda na kuwa na mageuzi makubwa kwenye viwanda.
Aidha aliagiza Shirika Hilo kutoa taarifa ya maeneo yote ya wazi wanayo miliki na kubainisha shughuli zinazofanyika na kama yana tija kwa Shirika Hilo na kama sio ushauri utolewe.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SIDO, Profesa Sylvester Mpanduji amesema  wamejipanga kwenda kutekeleza agizo la ujenzi wa viwanda 20 Kila mkoa na kuwataka wananchi kununua bidhaa zinazozalishwa nchini Ili kukuza viwanda hivyo.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.