MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Shirikianeni kutekeleza majukumu- Possi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Shirikianeni kutekeleza majukumu- Possi
Habari

Shirikianeni kutekeleza majukumu- Possi

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

WAJUMBE wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) wametakiwa kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yao kwa wakati ili kufikia malengo waliyojiwekea ndani ya muda uliopangwa.

Wito huo umetolewa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi wakati wa kikao chake cha kwanza na Menejimenti ya Ofisi hiyo tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Dkt. Possi amesema kuwa malengo ya kikao hicho ni kufahamiana, kuwekana sawa na kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya kila siku na kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo, Dar es Salaam.

“Tufanye kazi kwa ushirikiano kwa muda wote, mtu anapokwama apewe ushirikiano, tusing’ang’anie kanuni tu za utumishi, ila haimaanishi tuvunje kanuni na taratibu za Serikali, tupunguze kufuata milolongo isiyo ya lazima ili tuweze kutekeleza majukumu kwa wakati na kubadilika badala ya kufanya kazi kwa mazoea,” amesema Dkt. Possi.

Pia, ameongeza kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imekasimiwa majukumu ya kuratibu, kusimamia na kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa niaba ya Serikali na taasisi zake hivyo amewataka wajumbe wa Menejimenti kuishauri Serikali kwa wakati kuhusu uendeshaji wa mashauri mbali mbali ili kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama za uendeshaji wa mashauri na ulipaji wa fidia.

Vile vile ametoa wito kwa menejimenti hiyo kuzingatia mawasiliano kwa kuwa mawasiliano ni muhimu, mawasiliano yafanyike kwa wakati na watoe mrejesho wa hatua za utekelezaji wa majukumu, na wazingatie mnyororo wa kufanya maamuzi kwa kuwa ni muhimu ndani ya Serikali.

Naye Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Alice Mtulo akisoma taarifa ya utekelezaji ya Ofisi hiyo kwa Dkt. Possi ameahidi kumpa ushirikiano na kutekeleza maelekezo na miongozo yote aliyoitoa ili kuongeza tija na ufanisi katika kuhudumia wananchi na kuiwakilisha Serikali na taasisi zake katika uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi ndani na nje ya nchi.

Dkt. Possi amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini, kumteua na kumuapisha kuwa Wakili Mkuu wa Serikali yeye na Bi. Mtulo na wote wako tayari kutekeleza majukumu waliyokasimiwa na Serikali.

You Might Also Like

SOKO LA MADINI LA 43 LA ZINDULIWA TUNDURU RUVUMA.

Wananchi Washauriwa Kujiunga Na Chuo Cha Ualimu Na Ufundi Stadi Morogoro

Miradi Ufungaji Mifumo Ya Umeme Jua 20,000 Mbioni Kuanza

UDOM Yatumia Akili Mnemba Kugundua Dawa

Wataalamu wa Tanzania, Kenya Watoa Ufafanuzi Kuhusu Maana Na Matarajio Ya Jumuiya Ya China, Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TASAC yahadharisha wavuvi, wasafirishaji majini kuhusu upepo mkali
Next Article Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji utakaoongeza thamani ya Madini nchini
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbegu Bora za Miwa Zenye Tija ya Tani 200 kwa Hekta Zaendelea Kuwanufaisha Wakulima
Habari August 7, 2025
Mbegu Bora za Mpunga Zazalishwa TARI Dakawa, Ifakara
Habari August 7, 2025
Mtego wa Inzi Wa Matunda Suluhisho Salama kwa Wakulima
Habari August 7, 2025
Mafua, Kifua Yadaiwa Kusababisha Kifo cha Job Ndugai
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?