MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Shilingi bilioni 4.6 kupeleka umeme maeneo ya migodi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Shilingi bilioni 4.6 kupeleka umeme maeneo ya migodi
Habari

Shilingi bilioni 4.6 kupeleka umeme maeneo ya migodi

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali imetenga takribani sh bilioni 4.6 kupeleka umeme kwenye maeneo ya migodi mkoani Ruvuma.

Kapinga ameyasema hayo leo Agosti 18, 2024 wakati akizindua Kituo cha Mauzo ya Makaa ya Mawe ya kampuni ya Market Insight Limited (MILCOAL), inayojihusisha na uchimbaji, uuzaji na usambazaji wa Makaa ya Mawe, Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

“Hapa katika mgodi wa MILCOAL tutatumia zaidi ya shilingi milioni mia mbili kuleta umeme, nguzo tayari zimeshawekwa na sasa hivi wataalam wameanza kazi ya kuvuta waya.” Amesema Kapinga

Ameongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati inatekeleza miradi ya kupeleka nishati ya umeme kwenye maeneo makubwa ya uwekezaji ikiwemo migodini.

Kapinga amesisitiza kuwa makaa ya mawe ni chanzo cha nishati thabiti na ya kutegemewa katika maeneo ya uwekezaji mkubwa hususani viwandani.

Amewapongeza MILCOAL kwa uwekezaji huo ambao unachangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Amewahakikishia wawekezaji kuwa, Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji ikiwemo ujenzi wa miundombinu wezeshi na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inathamini wawekezaji.

Kuhusu Kampuni kuwajibika kwa jamii inayozunguka Kapinga amesema Sera za Nishati na Madini zinatambua uwajibikaji wa Kampuni kwa jamii zinazozunguka miradi na hivyo ameitaka Kampuni ya MILCOAL kutekeleza suala hilo ipasavyo.

You Might Also Like

Halmashauri Zahimizwa Kujenga Viwanda Vya Michezo.

Asha Moto Aibuka Kidedea Ubunge wa Viti Maalum Mtwara Kupitia CCM

IITA Kuleta Mabadiliko Ya Kilimo Afrika

Bahari  Ina Fursa Nyingi Zisizofahamika-Tasac

China Yafundisha Wanafunzi DIT kuzifikia fursa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wakandarasi Miradi wa  TAZA Watakiwa Kukamilisha Kazi kwa Wakati 
Next Article Tanzania Mwenyeji Mkutano wa Mafuta na Gesi, 2025
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbegu Bora za Miwa Zenye Tija ya Tani 200 kwa Hekta Zaendelea Kuwanufaisha Wakulima
Habari August 7, 2025
Mbegu Bora za Mpunga Zazalishwa TARI Dakawa, Ifakara
Habari August 7, 2025
Mtego wa Inzi Wa Matunda Suluhisho Salama kwa Wakulima
Habari August 7, 2025
Mafua, Kifua Yadaiwa Kusababisha Kifo cha Job Ndugai
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?