MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali yazindua Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii na ‘Hifadhi Scheme’ kwa Waliojiajiri
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali yazindua Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii na ‘Hifadhi Scheme’ kwa Waliojiajiri
Habari

Serikali yazindua Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii na ‘Hifadhi Scheme’ kwa Waliojiajiri

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
4 Min Read
Na Mwandishi Wetu 
ARUSHA: SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano imezindua Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii pamoja na Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wananchi Waliojiajiri ‘Hifadhi Scheme’ hatua inayolenga kupanua wigo wa hifadhi ya jamii na kuongeza ushirikishwaji wa wananchi katika mifumo ya kinga ya kijamii.
Uzinduzi huo umefanyika Februari 9, 2026 katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya kinga ya jamii uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), ukiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Habari Picha 11155
Akizungumza katika hafla hiyo, Sangu amesema sera hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma jumuishi za hifadhi ya jamii.
Ameongeza kuwa tangu 2018, Serikali imefanya maboresho ikiwemo kuunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kubaki na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Wafanyakazi wa Huduma za Umma (PSSSF) ili kuongeza ufanisi wa huduma na ulipaji wa mafao.
Habari Picha 11156
Sangu amesema maboresho hayo yameongeza idadi ya wanachama, NSSF imeongezeka kutoka wanachama 808,935 mwaka 2020 hadi zaidi ya wanachama 2,213,659 mwaka 2025, huku PSSSF ikiongezeka kutoka 697,677 hadi 899,948.
Aidha, thamani ya uwekezaji wa Mifuko imeongezeka kutoka Sh. Trilioni 9.36 hadi Trilioni 20.14, na jumla ya thamani ya Mifuko kufikia trilioni 24.20.
Habari Picha 11157
Kuhusu mpango wa Hifadhi Scheme, alisema hadi Desemba 2025 zaidi ya wanachama 500,000 kutoka makundi mbalimbali yakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiriamali wamejiunga, huku lengo likiwa kufikia wanachama milioni 5.5 ifikapo Juni 2031.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mary Maganga, amesema Serikali imeipa NSSF jukumu la kupanua wigo wa hifadhi ya jamii kwa wananchi waliojiajiri ili kuhakikisha sera mpya inaleta matokeo yanayotarajiwa.
Habari Picha 11153
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Masha Mshomba, amesema Mfuko unaendelea kuboresha utoaji wa huduma, kuongeza uandikishaji wa wanachama wapya, na kupanua wigo wa uwekezaji ndani na nje ya nchi, ikiwemo nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Afrika Mashariki.
Mshomba amesema Mfuko umepata mafanikio makubwa katika Serikali ya awamu ya sita ambapo thamani ya NSSF imeongezeka kutoka Trilioni 4.8 mwaka 2021 hadi Trilioni 10.4 Desemba 2025, na kuwa imepata ziada kwa miaka minne mfululizo kuanzia 2021 hadi mwaka wa fedha 2024/25, ikivuka lengo la ziada ya Sh.Trilioni moja.
Habari Picha 11161
Akizungumzia ukusanyaji wa michango, Mshomba amesema Mfuko umeendelea kuvuka malengo, ambapo mwaka wa fedha 2023/24 ulifikia zaidi ya Sh. Trilioni mbili, huku mwaka 2024/25 makusanyo yakizidi Trilioni 2.4 na kwamba katika kipindi cha miaka mitano mfululizo kuanzia 2020 hadi 2025, NSSF imefanikiwa kuvuka lengo la kukusanya angalau shilingi trilioni moja kwa mwaka.
Mshomba ameongeza kuwa mafanikio hayo yamechangiwa na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Habari Picha 11158
NSSF ina zaidi ya wanachama milioni 2.3 na imejikita kuboresha huduma kupitia TEHAMA na mpango wa miaka mitano unaolenga kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa 2050 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Habari Picha 11159

You Might Also Like

Ufanisi Wa TANESCO Katika  Utekelezaji Na Usimamizi Wa Miradi Umeleta Mfumo Madhubuti Wa Nishati- Ndejembi

Kasi Ya Kusambaza Umeme Kwenye Vitongoji Yaanza-Kapinga

Washauri Serikali Kutumia Fedha Za Miradi

Mpogolo Aipongeza Halmashauri Maandalizi Mikopo Asilimia 10

Watumishi wa Umma Watakiwa Kuwa na Nidhamu, Ubunifu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article CWT Yaiomba Serikali Kurekebisha Sheria za Vyama vya Wafanyakazi
Next Article Makamu wa Rais Azindua Mpango wa Kukuza Ujuzi, Ajira kwa Vijana
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Makamu wa Rais Azindua Mpango wa Kukuza Ujuzi, Ajira kwa Vijana
Habari February 9, 2026
CWT Yaiomba Serikali Kurekebisha Sheria za Vyama vya Wafanyakazi
Habari February 9, 2026
Serikali Yazindua Soko Kuu Jipya la Kariakoo Baada ya Moto wa 2021
Habari February 8, 2026
TALGWU Yaipongeza Timu Ya Makatibu Wa Mikoa Na Mawakili Wa Kanda Kwa Kutoa Huduma Bora Kwa Wanachama
Habari February 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?