MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yaimarisha Vitengo vya Tathmini na Ufuatiliaji Kuwa Huduma Bora kwa Wananchi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yaimarisha Vitengo vya Tathmini na Ufuatiliaji Kuwa Huduma Bora kwa Wananchi
Habari

Serikali Yaimarisha Vitengo vya Tathmini na Ufuatiliaji Kuwa Huduma Bora kwa Wananchi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaendelea kuimarisha vitengo vya tathmini na ufuatiliaji katika kila wizara ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Akijibu swali la Mbunge wa Monduli, Isack Copriano, aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuimarisha timu hizi ili kuharakisha majibu kwa wananchi na kero zao, Dkt. Nchemba alisema vitengo hivyo vitapewa rasilimali za kutosha.
“Kwenye kila wizara, kuna hivi vitengo vya ufuatiliaji na tathmini. Tunapanga kuongeza bajeti zao ili viweze kutimiza wajibu wao katika ufuatiliaji wa miradi na shughuli zote za Serikali,” alisema.
Dkt. Nchemba pia alibainisha hatua nyingine za kuimarisha mawasiliano na wananchi, ikiwemo kuanzishwa kwa kituo cha kupokea simu (Call Centre) namba 190, ambacho kinawapa wananchi nafasi ya kutoa kero zao na kupata majibu moja kwa moja.
Aidha, Waziri Mkuu alisema Serikali inalenga kurejesha utaratibu wa kila kiongozi kubeba hoja za wananchi kupitia rejesta maalumu, zitakazotumika katika ofisi za viongozi kurekodi kero na kutoa mrejesho serikalini kila mwisho wa mwezi.
“Utaratibu wa kupokea kero siyo wa kwenye ziara tu. Kila mwezi viongozi watapaswa kutoa taarifa ya idadi ya wananchi waliowahudumia, majibu waliyoyatoa, namba za simu za wananchi waliowahudumia na jinsi hoja hizo zilivyotatuliwa,” alisisitiza.
Dkt. Nchemba aliongeza kuwa, lengo ni kuhakikisha wananchi hawatahitaji kwenda kutafuta majibu kwa viongozi, bali hoja zao zinashughulikiwa ipasavyo na kuripotiwa kwa ufanisi.

You Might Also Like

Miradi iliyokamilika ianze kutoa huduma- Nyamoga

Mchengerwa Apongeza Shule Ya Sekondari Kibaha Kwa Ufaulu Wa Hali Ya Juu

Kimwaga Mwenyekiti Mpya DCPC, Ahimiza Nidhamu

Bil 67 Zatumika Kujenga Barabara, Masoko  Mwanza-Profesa Shemdoe

Tanzania, Afrika Kusini Zakubaliana Kuharakisha Makubaliano ya Ushirikiano

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kanzidata ya Taifa ya Uwekezaji Yalenga Kuboresha Takwimu na Kuvutia Wawekezaji
Next Article Ikomba: Acheni Makundi, Jengeni Umoja wa Chama
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ubunifu Wa Majengo Watakiwa Kuzingatia Tija Na Gharama Nafuu
Habari April 11, 2026
Waziri Ulega aridhishwa na miradi ya dharura TANROADS
Habari April 11, 2026
Mbunge Majule ataka wanawake wapewe elimu ya fedha na mitaji
Habari April 11, 2026
Mbunge Msita Ataka Ukarabati Wa Haraka Barabara Zilizoharibiwa Na Mvua
Habari April 11, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?