MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Kumuenzi Mzee Morris, Ngoma Zake 10
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Kumuenzi Mzee Morris, Ngoma Zake 10
Habari

Serikali Kumuenzi Mzee Morris, Ngoma Zake 10

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Danson Kaijage.

DODOMA: WAZIRI wa Habari, Utamaduni,    Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Serikali inatambua, inathamini michango mikubwa ya wabunifu na itaendelea kuwaenzi akiwemo Mzee Morrissi na ngoma zake 10.

Profesa Kabudi amesema hayo Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.

Amesema utakapomalizika ujenzi mkubwa wa Shirika la Utangazaji TBC kutakuwa na sehemu muhimu ya makumbusho ambayo yataonyesha kazi zilizofanywa na wabunifu hao pamoja na ngoma 10 za mzee Morris.

Pia amesema katika kupiga ngoma zake ambazo husikiwa na shirika la utangazaji la TBC wakati wa kutangaza saa au taarifa ya habari ni sehemu muhimu ya kumuenzi.

Kabudi amesema Tanzania ndiyo nchi pekee yenye anuai kubwa ya Utamaduni na lugha Barani Afrika.

Amesema kwa upande wa Lugha Tanzania ndiyo yenye makundi yote ya lugha mengi kuliko nchi yoyote Afrika.

“Tuna makundi ya lugha ya kibantu ukichukua Afrika ya Magharibi wote ni wa bantu, tunaweza kuwa na makabila 600 lakini wote ni wabantu.

“Lakini sisi tuna makabila ambayo asili yao ni kibantu,wengine ni Waniloti na Waniloti ni makundi mawili kwenye Mbuga yani Wamasai na wale wa kwenye mito Wajaruo.

“Lakini pia sisi tunao Wakoisani wapo Kondoa,Ovada mpaka Manyoni,lakini sisi pia tunawatu wanaozungumza lugha za Kiafloatiki ni Wairaq na Wamburu,” amesema.

Ameeleza Tanzania ndiyo nchi ambayo ina mshikamano na umoja mkubwa kuliko nchi yoyote Barani Afrika Kusini mwa Sahara kwa sababu Tanzania sasa ni Taifa siyo mkusanyiko wa makabila na Rais  Samia Suluhu Hassan aliendeleza hilo.

“Lakini pamoja na umoja huo tunaouona bado sisi ndiyo wenye anuai kubwa ya Utamaduni na lugha ambazo hazifanani lakini tumewekwa pamoja kama Taifa,” amesema.

You Might Also Like

Mtanda Akagua Maendeleo Ya Mradi YA Hoteli Ya Nyota Tano Ya NSSF

Kongamano la Kahawa Bora Afrika kufanyika Tanzania Februari mwakani

Rais Samia kufungua mkutano wa Mawaziri wa Uvuvi

TMDA Kudhibiti Bidhaa Za Tumbaku Ili Wananchi Wasiendelee Kupata Madhara

Chanzo Cha Bunge Kuridhia Hoja Ya Wanaojifungua Njiti, Kilianzia Hapa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Awamu Ya Pili Uboreshaji, Uwekaji Wazi Wa Dafatri La Wapiga Kura Kuanza Mei
Next Article Kabudi Aelezea Mafanikio Ya Wizara Yake
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tume ya Kurekebisha Sheria Yaelimisha Umma Kuhusu Haki za Wanyama
Habari August 6, 2025
Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima
Habari August 6, 2025
Ofisa wa TARI Kuwapo Kila Kituo cha Umwagiliaji – Naibu Katibu Mkuu
Habari August 6, 2025
Mbinu Mpya za Kilimo kwa Vijana Zapata Umaarufu Nanenane Banda La VETA
Habari August 6, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?