MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: SEforALL Kuimarisha Ushirikiano Upatikanaji Nishati Endelevu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > SEforALL Kuimarisha Ushirikiano Upatikanaji Nishati Endelevu
Habari

SEforALL Kuimarisha Ushirikiano Upatikanaji Nishati Endelevu

Author
By Author
Share
4 Min Read

Na  Mwandishi Wetu

VIONGOZI  mbalimbali wanaoshiriki mkutano wa kimataifa kuhusu matumizi ya nishati endelevu kwa watu wote unaofanyika nchini Barbados wameshauri kuimarishwa kwa ushirikiano wa kikanda na kimataifa ili kuwezesha upatikanaji wa nishati endelevu kwa gharama nafuu.

Akizungumza katika mkutano  huo unaofanyika jijini Bridgetown, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania kwa upande wake chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan, imepanga kuwawezesha asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Amesema, kupitia mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) unaozalisha megawati 2,115 utawezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika na endelevu kwa maendeleo na ustawi wa wananchi katika ngazi mbalimbali.

Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, utekelezaji wa lengo namba saba katika mpango wa maendeleo ya milenia unahitaji ushirikiano miongoni mwa Serikali na sekta binafsi katika kuboresha upatikanaji wa nishati safi ikiwa ni moja ya utatuzi wa changamoto zilizopo.

Amesema ni muhimu kwa mataifa kuwekeza katika miundombinu kwa ajili ya upatikanaji wa nishati safi sambamba na kuweka mifumo ya ubunifu na utashi katika kuwezesha upatikanaji wa nishati kwa usawa bila kuacha makundi mengine.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mtendaji Mkuu SEforALL, Damilola Ogumbiyi, amesema zinahitajika ajenda madhubuti za kuwezesha kukabiliana na vitendo vinavyotokana na matumizi ya nishati isiyo safi

“ Tumeshuhudia matokeo yanayosababishwa na ukosefu wa nishati safi kama vile uharibifu wa mazingira unaosababisha ukame na mafuriko ambayo kwa kupata nishati safi tunaweza kuondokana nayo,” amesema.

Naye, Waziri Mkuu wa Barbados,  Mia Mottley amesema ni wakati sasa wa kuweka mkakati wa kimataifa na kukubaliana kushirikiana kumaliza changamoto ya upatikanaji wa nishati kwa wote.

Akizungumzia mkutano wa misheni 300 (M300) uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mia amesema inatia simanzi kuwa na watu zaidi ya milioni 600 barani Afrika wanaishi bila huduma ya umeme suala ambalo limesababisha changamoto katika nchi nyingi duniani.

“Tunahitaji kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo, uwe ufumbuzi wa ndani au kutoka katika nchi yoyote duniani,” amesema  Mottley.

Kwa upande wake, Rais wa Sierra Leone,  Julius Maada Bio amesema katika kipindi hiki ambapo nishati ni nyenzo muhimu katika upatikanaji wa maendeleo, ni muhimu kuwezesha watu na makundi yote kupata nishati hususani katika maeneo ya vijijini yanayokabiliwa na umasikini uliokithiri.

“Wanawake na watoto ambao wanatumia muda mwingi kutafuta nishati ambayo sio safi kwa ajili ya kupikia, wanatakiwa kuwezeshwa kupata nishati safi na hivyo kutumia muda mwingi kufanya shughuli za maendeleo,” ameongeza.

Mkutano huo wa kimataifa ni mwendelezo wa mikutano ya kikanda na kimataifa inayokusudia kupata suluhisho la changamoto zinazotokana na matumizi ya nishati chafu.

Januari, 2025, viongozi na wakuu wa nchi mbalimbali barani Afrika na taasisi mbalimbali za fedha ikiwemo Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika walikutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafuta uwezekano wa kuwawezesha watu takribani milioni 300 barani Afrika kupata huduma ya nishati ya umeme.

You Might Also Like

NEMC Kupambana Na Magugu Maji Ziwa Victoria

Ridhiwani Ashiriki Kikao Cha Kazi Na Ajira Saudi Arabia

Ridhiwani Kikwete aziita sekta binafsi kushirikiana na serikali,  apokea vifaa tiba na madawati kutoka NMB

Aloe Dorotheae, Mmea Unaopatikana Tanzania Pekee

Japan Yatoa Bilioni 27 Kuboresha Sekta Ya Afya

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Taasisi Za Dini Zinazofanya Biashara Zinatakiwa Kulipa Kodi
Next Article Kamati Ya Bunge Yahimiza Maslahi Ya Watumishi Wapya Yazingatiwe
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?