MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ridhiwani: Ili Kufikia Muafaka Masuala Ya Kazi, Serikali Inahimiza  Vyombo Vya Mashauriano
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ridhiwani: Ili Kufikia Muafaka Masuala Ya Kazi, Serikali Inahimiza  Vyombo Vya Mashauriano
Habari

Ridhiwani: Ili Kufikia Muafaka Masuala Ya Kazi, Serikali Inahimiza  Vyombo Vya Mashauriano

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DODOMA: WAZIRI Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema serikali inahimiza matumizi ya vyombo vya mashauriano ili kuzungumza na kufikia mahali pazuri kwenye masuala yahusuyo wafanyakazi.

Ridhiwani amesema hayo alipokuwa akizindua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), jijini Dodoma.

Akizungumzia vyombo hivyo amevitaja kuwa ni Bodi ya Ushauri wa Masuala ya Kazi, Uchumi na Kijamii (LESCO), Bodi ya Mishahara pamoja na Mabaraza ya Wafanyakazi ili kuweza kuzungumzia masuala ya wafanyakazi na kufikia muafaka.

Pia Waziri Ridhiwani amesema mabadiliko ya sheria mbalimbali yanaendelea ikiwemo suala la Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), kwamba ni moja kati ya sheria zilizoguswa.

“Timu ya wataalamu ipo Morogoro ikifanya mapitio mbalimbali ya sheria na kanuni zinazohusu vyama vya wafanyakazi. Itakapokuwa tayari tunakuja kuwashirikisha tukitambua ninyi ni wadau muhimu.

“Mabadiliko ya sheria tunayotaka kuyafanya na mapitio ya kanuni tunayoendelea kuyafanya nina imani kwa namna moja au nyingine yanagusa maslahi ya wafanyakazi.

“Na ninyi kama chama kinachosimamia maslahi hayo ni muhimu kushirikishwa na ili sheria iweze kuwa na tafsiri ambayo inakusudiwa,” amesema.

Awali Katibu Mkuu TUCTA, Hery Mkunda alimweleza Waziri Ridhiwani kwamba, mwaka 2018/19 Sheria ya Utumishi wa Umma rejeo la 2019 ilifanyiwa marekebisho yanayomnyima mtumishi wa umma haki ya kutumia mfumo wa CMA na mahakama katika kutatua mgogoro wa kikazi.

Amesema mabadiliko hayo yamesababisha athari kubwa kwa watumishi wa umma. Hivyo TUCTA inapendekeza milango ya majadiliano ifunguliwe ili yafanyike marejeo ya sheria hiyo lengo likiwa mtumishi wa umma kurejeshewa haki yake ya kuamua mfumo atakaoona unafaa kutatua mgogoro wake, jambo ambalo Waziri Ridhiwani tayari amelitolea ufafanuz

You Might Also Like

Makamanda Wa Polisi Msiende Nyumbani na Vyeo Vya Ukamanda

TPHPA Yaelekeza Wakulima Kutumia Viuatilifu Kwa Usahihi

Ajali ya treni Kigoma , abiria 70 wajeruhiwa

Serikali Yapambana Kutokomeza Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele

CCCC Yakutana na Wanahabari, Yapanga Mikakati Mipya 2025

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ridhiwani Apongeza Kurudi Kwa Gazeti La Mfanyakazi TANZANIA
Next Article Wafanyakazi Wakumbushwa Kujitokeza. Kwa Wingi Kupiga Kura
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wadau Wakaribishwa Kuwekeza Katika Uchakataji, Biashara ya Mkonge Nchini
Habari August 7, 2025
Mramba Afungua Mafunzo Ya Teknolojia Ya Nishati Jua Kwa Watalaam
Habari August 7, 2025
Mbegu Bora za Miwa Zenye Tija ya Tani 200 kwa Hekta Zaendelea Kuwanufaisha Wakulima
Habari August 7, 2025
Mbegu Bora za Mpunga Zazalishwa TARI Dakawa, Ifakara
Habari August 7, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?