Na Mwandishi Wetu
PWANI: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amezungumza na Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na wajumbe wa Halmashauri za Vijiji wapatao zaidi ya 1900 eneo la Lugoba, Chalinze leo Novemba 30, 2024.

“Nimetumia nafasi hiyo kuwakumbusha wajibu wao kwa Wananchi, Serikali zao na kwa Chama Chao. Pia nimewatakia kheri katika majukumu yao kwa jumla na kuwaahidi ushirikiano mkubwa sana toka kwangu na ofisi yangu,” amesema.
