Na Mwandishi Wetu
DODOMA: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amepata nafasi ya kutembelea Kituo cha Kulelea watoto cha Kikombo, kilichopo Dodoma.
Kituo hicho kipo chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Katika ziara hiyo pamoja na kuona maendeleo ya kituo pia amekabidhi Vyerehani Kwa hisani ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa ajili ya kujifunza kushona.