Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete ametembelewa na ugeni wa Watendaji wa Benki ya NMB wakiongozwa na Meneja Mahusiano Vicky Bishubo.
Ridhiwani amesema lengo la wageni hao ni kujitambulisha na kutambulisha bidhaa mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo.
Amesema ameweza kutambulisha baadhi ya maeneo benki hiyo inaweza kushirikiana na Serikali katika kufanikisha uwezeshaji Vijana na Jamii.
#KaziInaendelea #UwezeshajiVijana