MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Rais Samia Awekeza Mabilioni Kuboresha Sekta ya Uvuvi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Rais Samia Awekeza Mabilioni Kuboresha Sekta ya Uvuvi
Habari

Rais Samia Awekeza Mabilioni Kuboresha Sekta ya Uvuvi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Profesa Mohamed Sheikh Akagua Gati la Kuegeshea Meli la Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)
Na Lucy Ngowi
SERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango wa kimkakati wa kuibadilisha sekta ya uvuvi nchini, ikilenga kuifanya kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi.
Mpango huo unajumuisha ununuzi wa meli za uvuvi wa bahari kuu, upanuzi wa ufugaji wa viumbe wa maji, na ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya uvuvi.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia sekta ya uvuvi, Profesa Mohamed Sheikh, alisema serikali tayari imenunua meli moja ya uvuvi ambayo ipo katika maji ya Tanzania na itaanza shughuli zake mara baada ya kukamilika kwa taratibu za mwisho.
Aidha, meli nyingine nne ziko katika hatua mbalimbali za manunuzi ili kuongeza uzalishaji wa samaki katika bahari kuu.
Profesa Sheikh alisema uwekezaji huu ni sehemu ya dira ya dhati ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuibadilisha sekta ya uvuvi kutoka kujikimu hadi kuwa sekta yenye uzalishaji mkubwa, itakayochangia ukuaji wa uchumi na kuongeza mapato ya kigeni.
Kwa sasa sekta ya uvuvi inachangia takribani asilimia 1.8 ya Pato la Taifa, lakini serikali inalenga kuongeza mchango huo hadi angalau asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.
Moja ya mikakati muhimu ni kuendeleza ufugaji wa samaki, ambavyo kwa sasa vinachangia takribani asilimia 7 ya uzalishaji wa samaki, huku asilimia 93 ikitokana na uvuvi wa asili unaokabiliwa na changamoto kama uvuvi haramu, ongezeko la idadi ya watu, na mabadiliko ya tabianchi.
Serikali inalenga pia kuzalisha vifaranga bora vya samaki, kuongeza aina za samaki zinazofugwa, na kuvutia wawekezaji.
Tanzania ina eneo la bahari lenye kilomita za mraba 223,000, sawa na asilimia 45 ya ukubwa wa nchi.
Kutumia rasilimali hii kikamilifu kutasaidia kuongeza uzalishaji wa samaki, kukuza uchumi, na kuboresha lishe ya wananchi.
Pia, ujenzi wa bandari za kisasa za uvuvi Kilwa Masoko na Bagamoyo unatarajiwa kuongeza uwezo wa huduma katika sekta hii.
Profesa Sheikh alibainisha kuwa uwekezaji huu utasaidia kuimarisha Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), kuhakikisha meli za taifa zinamilikiwa na kuendeshwa, kupunguza utegemezi wa meli za kigeni, na kuhakikisha mapato yanazunguka ndani ya nchi.

You Might Also Like

Tembo Wasaidia Kueneza, Kuotesha Mimea Asilia

TUCTA: Wafanyakazi Jitokezeni  Kwa Wingi Kwenda Kupiga Kura Mchague Viongozi Watakaolinda  Maslahi Yenu  

Serikali Yasisitiza Utoaji Huduma Bora Utekelezaji Bima Ya Afya

Rais Samia kufanya ziara mkoani Morogoro, kuzindua safari za SGR

Mwongozo wa Mafunzo Elekezi Kwa Walimu Wapya Kazini Mbioni Kukamilika

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mkutano wa Mawaziri wa SADC Wahitimishwa Pretoria
Next Article Dawati  La Jinsia Unguja Latoa Ulinzi Na Usalama Kwa Watoto Wa Kike Kuwaepusha Na Ukatili
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Jamii Yatakiwa Kuzungumza Pamoja Kuhusu Maji, Masuala ya Jinsia
Habari March 16, 2026
Tume Ya Madini Yaweka Vipaumbele Kuwezesha Vijana Kushiriki Katika Uchimbaji Madini 
Habari March 16, 2026
Dawati  La Jinsia Unguja Latoa Ulinzi Na Usalama Kwa Watoto Wa Kike Kuwaepusha Na Ukatili
Habari March 16, 2026
Mkutano wa Mawaziri wa SADC Wahitimishwa Pretoria
Habari March 13, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?