Na Mwandishi Wetu
RAIS Samia Suluhu Hassan amewasili Harare Nchini Zimbabwe ambako atashiriki Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Katika Mkutano huo utakao fanyika kesho Agosti 17, 2024 Rais Samia atapokea kiti cha Uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC kutoka kwa Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema.