MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ntonda Ameipongeza TEA Kwa Utekelezaji Bora Wa Miradi Ya Elimu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ntonda Ameipongeza TEA Kwa Utekelezaji Bora Wa Miradi Ya Elimu
Habari

Ntonda Ameipongeza TEA Kwa Utekelezaji Bora Wa Miradi Ya Elimu

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
´Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Methusela Ntonda ameipongeza Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo ya elimu kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa pamoja na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF).
Ntonda ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la TEA katika ufunguzi wa Maonesho ya Kitaifa ya Kazi za Utamaduni na Sanaa yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mkoani Dar es Salaam.
Akiwa kwenye banda hilo, Ntonda alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na TEA, zikiwemo taarifa za miradi ya elimu na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi, pamoja na bidhaa zilizotengenezwa na mmoja wa wanufaika aliyepata ufadhili wa kusomea Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi.
Vile vile Ntonda amevutiwa na juhudi za Mamlaka hiyo katika kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia, sambamba na uwezeshaji uliotolewa kwa watanzania kupitia ufadhili wa mafunzo ya ujuzi.
Amesema uwekezaji uliofanywa kupitia mifuko yote miwili una mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya sekta ya elimu na kukuza maarifa kwa wananchi, hasa vijana.
Pia amesisitiza umuhimu wa kuendeleza jitihada hizo kwa kushirikisha wadau mbalimbali ili kuhakikisha elimu bora na fursa za ujuzi zinapatikana kwa watu wengi zaidi nchini.
Awali, akitoa utambulisho wa Mamlaka hiyo, Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa TEA, Eliafile Solla alisema TEA ilianzishwa kwa lengo la kusimamia Mfuko wa Elimu wa Taifa, ambapo majukumu yake makuu ni kutafuta rasilimali fedha kutoka kwa wadau wa ndani na nje ya nchi,
 Kuzitumia kusaidia juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini. Aliongeza kuwa TEA pia ina jukumu la kuratibu na kusimamia utekelezaji wa miradi ya uendelezaji ujuzi kupitia Mfuko wa SDF.

You Might Also Like

VETA Shinyanga Yatumia Kompyuta Kubuni Bidhaa 

FCC Yatatua Kero 63  Za Walaji

Jengo la Uwekezaji la Wafanyakazi Kufunguliwa Novemba 

Rafiki Mkubwa wa Trump, Elon Musk atanufaika vipi baada ya kumuunga mkono?  

Dawati  La Jinsia Unguja Latoa Ulinzi Na Usalama Kwa Watoto Wa Kike Kuwaepusha Na Ukatili

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article JOWUTA : Waandishi Vitendeeni Haki Vyama Vyote
Next Article Spika Tulia Kufungua Kongamano La Uhuru Wa Wanataaluma Afrika UDSM
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Jamii Yatakiwa Kuzungumza Pamoja Kuhusu Maji, Masuala ya Jinsia
Habari March 16, 2026
Tume Ya Madini Yaweka Vipaumbele Kuwezesha Vijana Kushiriki Katika Uchimbaji Madini 
Habari March 16, 2026
Rais Samia Awekeza Mabilioni Kuboresha Sekta ya Uvuvi
Habari March 16, 2026
Mkutano wa Mawaziri wa SADC Wahitimishwa Pretoria
Habari March 13, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?