Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge, amesema ataunganisha Mbeya Mjini kuwa eneo moja linaloshirikiana.
Amesema hayo leo Novemba 12, 2025 katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Amesema maendeleo ya haraka yatawezekana iwapo wananchi watashirikiana kikamilifu.

“Muda wangu wa miaka mitano jimbo la Mbeya Mjini ni kusaidia wananchi kupata kipato. Miradi yote haiwezi kufanikishwa bila amani,” amesema Mwalulenge, akiwahimiza vijana kulinda utulivu wa jimbo hilo.
Mbunge amesema ajira kwa vijana na kufanya Mbeya kitovu cha uchumi ni sehemu ya ahadi zake ambazo anataka kuhakikisha zinafanikiwa.
Amesema kila hatua ya maendeleo ni kazi ya pamoja kati ya wananchi na viongozi.
Mwalunenge amedokeza kuwa anatarajia kushirikiana na Waziri Mkuu atakayethibitishwa pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa ufanisi.
Amesisitiza kuwa Mbeya mpya inahitaji mshikamano wa wananchi, viongozi na wadau wengine.

