Na Mwandishi Wetu
TABORA: MGOMBEA urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalim, amewaomba Watanzania kumwombea katika wiki hii ya mwisho kuelekea siku ya kupiga kura, Jumatano, Oktoba 29, 2025.
Akizungumza mjini Tabora, Mwalim amesema:
“Nawaombeni Watanzania, kila mmoja kwa imani yake awe Muislamu aniombee msikitini, na Wakristo wafanye hivyo makanisani. Naombeni dua ili nikichaguliwa niwe Rais asiye na kiburi wala majivuno, bali mwenye moyo wa utumishi.”
Aidha, aliwataka wakazi wa Tabora kuchagua CHAUMMA kama chaguo la mabadiliko na maendeleo ya kweli kwa taifa.

