MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mvua, Upepo Yaharibu Shule Lindi, Serikali Yatoa Milioni 96
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mvua, Upepo Yaharibu Shule Lindi, Serikali Yatoa Milioni 96
Habari

Mvua, Upepo Yaharibu Shule Lindi, Serikali Yatoa Milioni 96

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, amesema kuwa Sh.Milioni 96 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Msingi Mkwajuni mkoani Lindi, iliyoharibiwa na mvua na upepo.
Profesa Shemdoe ameeleza hayo wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Nchinga, Salma Kikwete (CCM), aliyeeleza kuwa katika Shule ya Mkwajuni madarasa mawili yaliezuliwa na upepo, hali iliyosababisha wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo darasani.
Aidha, nyumba mbili za walimu pamoja na ofisi ya mkuu wa shule nazo ziliharibiwa.
Akijibu swali hilo, Profesa Shemdoe amesema tayari amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kufika katika shule hiyo na hatua za awali zimechukuliwa.
“Tayari nimemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kwenda katika Shule ya Mkwajuni, na ameshakwenda. Kiasi cha Sh. Milioni 96 kimeshapelekwa kwa ajili ya kurekebisha madarasa yaliyoathirika.
“Serikali tayari imelichukua jambo hili, na nimshukuru Naibu Waziri wa Elimu kwa namna alivyolielezea,” amesema Profesa Shemdoe.
Waziri huyo pia ametoa pole kwa wananchi wa Nchinga, hususan wakazi wa Kijiji cha Mkwajuni, kutokana na tukio hilo.
Awali, Mbunge wa Nchinga, Salma Kikwete, alitoa pole kwa wananchi wa eneo lake kutokana na kadhia iliyotokea Januari 29, 2026, katika Shule ya Mkwajuni.
Amehoji kauli ya Serikali pamoja na mkakati wa haraka wa kuhakikisha wanafunzi wanarejea shuleni na kuendelea na masomo yao.

You Might Also Like

Pinda Aitaka Jamii Kujikita Upandaji Miti Bila Kusubiri Matukio Maalumu

Polisi Dodoma Yawataka Wananchi Kutoa Taarifa 

Tanzania Yanadi Nishati Kimataifa

Biteko Amwakilisha Rais Samia Harambee Ujenzi Kanisa Katoliki

Trilioni 1.3  Zatumika Kuboresha Afya Ya Msingi Nchini

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mbunge Mgalu Auliza Hatima ya Ujenzi wa Chuo cha VETA Bagamoyo
Next Article Mtasingwa Aitaka Serikali Kuwatengea Eneo Wafanyabiashara wa Senene Bukoba
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ubunifu Wa Majengo Watakiwa Kuzingatia Tija Na Gharama Nafuu
Habari April 11, 2026
Waziri Ulega aridhishwa na miradi ya dharura TANROADS
Habari April 11, 2026
Mbunge Majule ataka wanawake wapewe elimu ya fedha na mitaji
Habari April 11, 2026
Mbunge Msita Ataka Ukarabati Wa Haraka Barabara Zilizoharibiwa Na Mvua
Habari April 11, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?