Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete, amesema serikali ipo katika hatua za mwisho za kuupeleka muswada wa wafanyakazi wa ndani, katika bunge linalokuja.
Ridhiwan amesema hayo Ofisini kwake alipotembelewa na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakaz Tanzaniai ( TUCTA), Tumaini Nyamhokya, Mhariri Mkuu wa Gazeti la MFANYAKAZI Shani Kibwasali pamoja na waandishi wa gazeti hilo.
Amesema, ” Katika moja ya jambo kubwa tunaenda kulifanya kisasa ni juu ya maisha ya mtumishi wa ndani.

“Kwamba unajua sasa hivi mimi nikikuchukua ukafanya kazi kwangu za ndani, utaishi ninavyotaka mimi, bila kujali pia mfanyakazi huyu wa ndani ana haki zake kama binadamu.
Ridhiwan Kikwete ameeleza inafikia sehemu wafanyakazi wa ndani, wanashindwa kuwaeleza waajiri wao kwamba wamepata mchumba kwa kuwa wakisema wanaogopa watafukuzwa kazi.
Amesema muswada huo ukipitishwa utawapa hadhi wafanyakazi wa ndani kwani watafanya kazi na kuishi kama wafanyakazi wa makundi mengine nchini.