Na Danson Kaijage
DODOMA: FATUMA Waziri amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) huku akiahidi kuendeleza mazuri yaliyofanywa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Anthony Mavunde.

Fatuma mwenye Elimu ya Shahada ya Uzamili kwenye Masuala ya afya amechukua fomu hiyo katika Ofisi za CCM, Wilaya ya Dodoma Mjini na kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya hiyo, Sophia Kabibi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu, amesema dhamira yake ni kuhakikisha anapaendeleza pale alipoishia aliyekuwa Mbunge wa Dodoma Mjini, Mavunde kwani amefanya kazi nzuri na ya kutukuka.