Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: DUKA Jipya la kwanza la Midea Group Afrika Mashariki limefunguliwa eneo la Mlimani City, Dar es Salaam.
Rais wa Midea MEA, Scott Fu amefungua duka hilo lenye Mita za Mraba 240.
Scott Fu amesema duka alilolifungua lina vifaa vyenye teknolojia inayotumia umeme mdogo ambavyo ni viyoyozi, friji, mashine za kuoshea, vifaa vya jikoni, vifaa vya nyumbani pamoja na bidhaa nyingine.
Amesema katika kuendeleza teknolojia mpya ya kasi ya 5G ulimwenguni, wanahitajika kubuni bidhaa nzuri na rafiki.
Pia amesema Midea Group itatoa mafunzo kwa wahandissi w kiufundi wa ndani zaidi ya 500 kwa miaka mitatu ijayo, ili kutoa fursa za ajira ikiwa ni pamoja na kukuza maendeleo ya kiuchumi Kikanda.
Amesema Midea Group imeshinda changamoto za masoko, “Midea Group kama Mchezaji bora katika Soko la Ushindani chini ya Uongozi wangu na Juhudi za pamoja na timu yangu, sehemu ya nje ya Midea imeongezeka kwa Mafanikio kutoka asilimia 24 hadi 29 na kiwango kimezidi bilioni 30 “.
Naye Ofisa Masoko wa kampuni hiyo, Miriam Zabron amesema ni furaha kubwa kwa kampuni hiyo kufungua duka eneo la Mlimani City.
Amesema wanakaribisha wananchi kuona bidhaa zilizopo na uzuri wake.
” Sisi ni namba moja kwa matumizi ya teknolojia. Tupo vizuri katika matumizi ya umeme mdogo na uimara wa bidhaa.
“Bidhaa zetu zinahimiki hata pale umeme unapoleta shida, tuna kiyoyozi kinachotumia umeme mdogo, ” amesema.
Amesema wana teknolojia tofauti tofauti, watanzania na dunia itafurahi kutumia umeme mdogo.
“Tunapunguza matumizi ya umeeme kwa kiasi kikubwa,” amesema.