Na Lucy Lyatuu
MFUKO wa Fidia Kwa Watumishi wa Umma (WCF) umesema Kwa Sasa mfanyakazi ndio mwemye dhamana ya kupeleka taarifa zake Kwa ajili ya kudai haki na zisichelewe ndani ya miezi 12.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF,Dk John Mduma amesema hayo jijini Dodoma alipotembelewa na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya Kwa ajili ya kutambulisha gazeti la MFANYAKAZI akiongozana pia na Mhariri Mkuu Shani Kibwasali.
Amesema kuna wafanyakazi wengi haki zao zinapotea na Kwa kushirikiana na MFANYAKAZI wanaweza kupata uelewa wa kutosha na kuchukua hatua mapema.
“Kuna Ile miezi 12 ya kutoa taarifa, na Mfanyakazi akichelewesha sheria inamkataza kupata haki yake,” amesema Dk Mduma.
Amesema Mfanyakazi akielimika atajua simu akipata Janga Atakuwa makini na mwajiri vilevile kuwa makini wakati mfanyakazi akitoa madai yake.
Dk Mduma amesema pia hivi karibuni sheria imepita kwamba vyama vya wafanyakazi au Mwanasheria wanaweza pia kupeleka taarifa na WCF wakarudi Kwa mwajiri.
Kwa upande,Rais Nyamhokya amesema kupitia chombo Cha MFANYAKAZI kitawezesha kundi hilo kujua Kila anayefidiwa na sheria mbalimbali zinazowahusu.
Naye Kibwasali amesema yapo mengi ya kujua kuhusu wafanyakazi na waelewe Taasisi zinazosimamia masuala yao.