MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mchengerwa Aongoza Ujumbe Wa Tanzania Kwenye Uzinduzi Wa Mkutano Wa Dunia Wa Tiba Asili
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mchengerwa Aongoza Ujumbe Wa Tanzania Kwenye Uzinduzi Wa Mkutano Wa Dunia Wa Tiba Asili
Habari

Mchengerwa Aongoza Ujumbe Wa Tanzania Kwenye Uzinduzi Wa Mkutano Wa Dunia Wa Tiba Asili

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu, New Delhi

WAZIRI  wa Afya,  Mohamed  Mchengerwa ameuongoza ujumbe wa Serikali ya Tanzania katika uzinduzi wa Mkutano wa pili wa dunia wa Tiba Asili unaoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye ukumbi wa kimataifa wa Bharat Mandapam jijini New Delhi India.

Mchengerwa amepongeza juhudi zinazofanywa na WHO za kuileta dunia pamoja ili kujadili suala la Tiba Asili na kupata ufumbuzi katika masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na utawala na udhibiti wa tiba asili, utafiti na ushahidi wa kisayansi, ujumuishaji wa tiba asili katika mifumo ya afya, matumizi endelevu ya raslimali za kiasili na uendelezaji wa raslimali watu kwenye eneo la Tiba Asili.

Habari Picha 10584

Mkutano huo umefunguliwa rasmi na  Prataprao Ganpatrao Jadhav, Waziri wa Nchi (Independent Charge), Wizara ya Tiba Asili (AYUSH), na Waziri wa Nchi, Wizara ya Afya na Ustawi wa Familia ya Serikali ya India, mbele ya  Jagat Prakash Nadda, Waziri wa Afya na Ustawi wa Familia wa Serikali ya India.

Hafla hiyo imewakutanisha Mawaziri, watunga sera wakuu, na wadau wa sekta ya afya kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akitoa hotuba yake kwa njia ya video kwenye ufunguzi huo amewasihi wajumbe wa mkutano huo kujadili kwa kina mada mbalimbali ili kubadilishana uzoefu na kwamba kwa sasa Tiba Asili bado itaendelea kuwa na mchango mkubwa kwa wanadamu kwa kuzingatia kuwa tiba asili ni sehemu ya tamaduni za watu katika mataifa yao.

Habari Picha 10585

 

Kando ya mkutano huo, Tanzania inatarajia kusaini Hati mbili za Makubaliano (MoU) na Serikali ya India kuhusu ushirikiano katika sekta ya afya na tiba asilia (Ayurveda), hatua itakayosaidia kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi, kuongeza uwezo wa rasilimali watu, na kuimarisha matumizi salama ya tiba asilia nchini.

Kusainiwa kwa hati hizo mbili za makubaliano ni hatua muhimu kwa Tanzania, kwani kutaimarisha ushirikiano wa kitaasisi na India katika maeneo ya kipaumbele ya sekta ya afya, kuongeza uwezo wa rasilimali watu wa sekta ya afya, kuimarisha udhibiti na matumizi salama ya tiba asilia, pamoja na kuchangia jitihada za Serikali katika kuimarisha mifumo ya huduma za afya na kufikia Bima ya Afya kwa Wote.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huu unaakisi dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya Afya katika kukuza tiba asilia salama, yenye ushahidi wa kisayansi na inayosimamiwa kwa misingi madhubuti ya udhibiti, sambamba na kuendeleza ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo endelevu ya afya kwa watu wote.

Mkutano huo wa siku tatu unatarajiwa kufungwa na Desemba 19, 2025 na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi, jambo linaloonesha uzito na umuhimu mkubwa wa mkutano huo katika ngazi ya juu ya kisera.

 

You Might Also Like

Wananchi Kutembea Mwendo Mrefu Kutokana Na Upungufu Wa Majengo

Wanataaluma Wahimizwa Kutumia Tafiti Kama Chachu ya Mabadiliko ya Jamii

Tume Ya Kurekebisha Sheria Tanzania Kuipitia Sheria Ya Takwimu

TPHPA Yanunua Ndege Kudhibiti Visumbufu Vya Mazao

Mbarawa Aagiza Matumizi Ya Kitufe Utambuzi Wa Dereva

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Katambi Aitaka NDC Kuleta Mapinduzi Makubwa Ya Viwanda
Next Article Kapinga Afichua Fursa Kubwa za Ajira na Biashara kwa Vijana Nchini Tanzania
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CAG Aipongeza TARURA Kwa Ujenzi Wa Miundombinu
Habari January 9, 2026
Tuna Deni La Kusimamia Miradi Na Kusikiliza Kero za wananchi Ili Kuleta Maendeleo Ya Kweli-Salome
Habari January 9, 2026
Rais Dkt Samia Azindua Majengo Ya Kisasa
Habari January 8, 2026
TEA, UNICEF Watekeleza Miradi ya Elimu Visawani Zanzibar
Habari January 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?