MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mbunge Ndoinyo Aitaka Serikali Kugawa Ngorongoro Kusogeza Huduma Karibu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mbunge Ndoinyo Aitaka Serikali Kugawa Ngorongoro Kusogeza Huduma Karibu
Habari

Mbunge Ndoinyo Aitaka Serikali Kugawa Ngorongoro Kusogeza Huduma Karibu

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Ngorongoro, Yanick Ndoinyo, ameishauri Serikali kugawa Wilaya ya Ngorongoro na kuboresha miundombinu yake ili kusogeza huduma karibu na wananchi.
Akichangia hotuba ya Waziri Mkuu bungeni Dodoma, amesema ukubwa wa wilaya hiyo unaofikia takribani kilomita za mraba 14,030 unasababisha wananchi kusafiri umbali mrefu, wakati mwingine hadi kilomita 300, kufuata huduma za msingi katika makao makuu ya wilaya.
Amesisitiza haja ya kuanzishwa kwa halmashauri mpya na maeneo mengine ya kiutawala ili kupunguza adha hiyo, akibainisha kuwa huduma kama vitambulisho vya NIDA, vyeti vya kuzaliwa na nyaraka nyingine zinapaswa kupatikana karibu zaidi na wananchi.
Kuhusu miundombinu, Ndoinyo ameeleza kuwa Ngorongoro bado haijaunganishwa na barabara ya lami kuelekea Arusha, hali inayokwamisha maendeleo.
Ametaja umuhimu wa ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu hadi Loliondo, akisema itapunguza muda wa safari kutoka saa 12 hadi chini ya saa tatu.
Katika sekta ya uchumi, amesema wilaya hiyo inategemea ufugaji, kilimo na utalii, huku akihimiza uwekezaji zaidi katika utalii ili kuongeza mapato kwa wananchi.
Pia amesisitiza kuwepo kwa mikakati ya kudumu ya upatikanaji wa malisho ili kulinda mifugo.
Kwa upande wa kilimo, ameeleza kuwa changamoto kubwa ni ukosefu wa masoko na miundombinu ya kuhifadhi mazao, hali inayosababisha hasara kwa wakulima.
Aidha, ameomba Serikali kusitisha kutaifisha mifugo na badala yake kutafuta suluhisho rafiki kwa wafugaji, huku akipongeza juhudi za Rais na Serikali katika kuimarisha maendeleo nchini.

You Might Also Like

Taasisi Za Umma Zasisitizwa Kuzingatia ubora Wa Mikataba Katika Utekelezaji Wa Majukumu Yao

Nchemba Afungua Mafunzo Ya PAC

Waziri Ulega aridhishwa na miradi ya dharura TANROADS

Ndege Ya TPHPA Yatua Rasmi Kudhibiti, Kwelea Kwelea, Viwavijeshi, Nzige 

Mgombea Udiwani Manyoni Adhalilishwa, Rushwa Yadaiwa Kuvuruga Kura Za Maoni

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ikomba: Acheni Makundi, Jengeni Umoja wa Chama
Next Article Mbunge Msita Ataka Ukarabati Wa Haraka Barabara Zilizoharibiwa Na Mvua
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ubunifu Wa Majengo Watakiwa Kuzingatia Tija Na Gharama Nafuu
Habari April 11, 2026
Mbunge Majule ataka wanawake wapewe elimu ya fedha na mitaji
Habari April 11, 2026
Mbunge Msita Ataka Ukarabati Wa Haraka Barabara Zilizoharibiwa Na Mvua
Habari April 11, 2026
Ikomba: Acheni Makundi, Jengeni Umoja wa Chama
Habari April 10, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?