Na Danson Kaijage
DODOMA: MAZAO ya Mbogamboga pamoja na vitunguu vinavyozalishwa nchini Tanzania ni sehemu ya maendeleo na kuchangia pato la taifa kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Latifa Mohamed Khamis, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema, “Mafanikio katika kipindi Maonesho ya Mbogamboga Expo Doha, 2023/24 Kampuni 13 zilishiriki na kufanikisha mauzo ya papo kwa papo ya Sh. Milioni 370,”.
Amesema fursa za mauzo za Sh. Milioni 125 zilifunguliwa kupitia mazungumzo ya kibiashara.
Pia amesema Kampuni za Qatar zilionesha nia ya kuwekeza katika usindikaji wa chakula na usimamizi wa taka.
Aidha amesema maonesho ya Biashara ya Afrika (AfCFTA Exhibitions on Intra-Africa Trade) ya mwaka 2023 ambapo,
Mauzo ya papo kwa papo yenye thamani ya Sh. Bilioni 2.17 yalifanyika na kuongeza kuwa Mikataba ya biashara yenye thamani ya Sh. Bilioni 17 ilisainiwa.

“Katika kipindi hiki, TanTrade imefanikiwa kupanua masoko, kusaidia biashara za Tanzania kupata fursa za kimataifa, kujenga uwezo wa wafanyabiashara wadogo na wa kati, na kuboresha mifumo ya upatikanaji wa taarifa.
Ameeleza kuwa uratibu wa DITF ambao umewezesha mafanikio kwa kipindi cha mwaka 2020/21 -2023/24,washiriki wa ndani wameongezeka kutoka 2,926 hadi 3,503, huku washiriki wa nje wameongezeka kutoka 76 hadi 451.