MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Manara: Sitapambana na Wafanyabiashara, Nitawatetea
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Manara: Sitapambana na Wafanyabiashara, Nitawatetea
Habari

Manara: Sitapambana na Wafanyabiashara, Nitawatetea

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MGOMBEA udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Haji Manara, ameahidi kuleta mageuzi ya kweli katika Kata ya Kariakoo ambayo ni kongwe na kitovu cha biashara nchini, kwa kushirikiana kwa karibu na wananchi na wafanyabiashara wa eneo hilo.
Manara ametoa ahadi hiyo alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni wa kata hiyo.
Amesema amerudi nyumbani Kariakoo kushirikiana na wananchi wake katika kutatua kero mbalimbali na kujenga Kariakoo wanayoitaka.
“Hii ni siku muhimu kwa ustawi wa Kariakoo. Nimerudi kushirikiana nanyi kujenga Kariakoo mpya, yenye maendeleo kwa wote. Kariakoo si kata ya kawaida, ni ya kipekee  ni kongwe, inaongoza kwa mapato nchini, na ni kitovu cha biashara Tanzania,” amesema Manara.
Pia amesema Kariakoo ni sehemu yenye historia kubwa, ikiwa ni moja ya maeneo ambapo harakati za ukombozi wa taifa zilifanyika, na kwamba kwa CCM ni kata mtambuka inayohitaji kiongozi makini atakayeunganisha makundi yote.
Habari Picha 9353
“Mimi sitakuwa diwani wa wakazi pekee wala wa wafanyabiashara peke yao. Nitakuwa diwani wa watu wote Kariakoo ni yetu sote. Bila wafanyabiashara, Kariakoo itasinyaa. Maendeleo hayawezi kutokea bila wao,” amesema.
Manara ameeleza kwamba hagombei nafasi hiyo kwa ajili ya kupambana na wafanyabiashara, kwani anapenda maendeleo na anaamini wafanyabiashara ni injini ya uchumi wa Kata hiyo.
Ameahidi kuwa biashara zitaendelea kufanyika kwa uhuru na kwa saa zote za siku na usiku, kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.
“Biashara zitafanyika hadi usiku kwa sababu si watu wote wana nafasi ya kununua mchana. Tutahakikisha tunashirikiana na polisi kudumisha usalama na kuruhusu biashara kufanyika kwa masaa mengi zaidi,” amesema.
Akigusia maendeleo yaliyofikiwa, Manara amesema miundombinu ya barabara katika Kariakoo imeboreshwa kwa zaidi ya asilimia 95, huku changamoto ya umeme ikianza kutatuliwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
“Kama umeme utakatika nikiwa diwani, mnapaswa kunipigia mimi. Mimi si kikwazo, bali ni daraja la maendeleo,” amesema.
Manara ameahidi hatawadhulumu wala kuwabughudhi wafanyabiashara wadogo, bali atahakikisha wanapewa heshima na mazingira bora ya kufanya biashara zao.
“Sitakuwa kikwazo. Nitasaidia kuwapigania wafanyabiashara wadogo wawe na hadhi yao katika jamii. Maendeleo ni kwa wote,” amesema.
Aidha, amewataka wakazi wa Kariakoo kumpigia kura yeye, pamoja na wagombea wengine wa CCM akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Pangani, Jumaa Aweso, akisema kuwa serikali ya awamu ya sita imefanya kazi kubwa na inastahili kuendelea kupewa nafasi.
“Tumshukuru Rais Samia. Serikali imetoa Sh. Bilioni 30 kwa ajili ya maendeleo ya Kariakoo. Hospitali yetu ya Mnazi Mmoja sasa ina kipimo cha kisasa cha MRI. Haya ni mafanikio makubwa. Msimuache Mama Samia, tumpe kura za kishindo asilimia 99.9,” amesisitiza.
Pia amempongeza  Mussa Zungu, kwa juhudi zake za kupigania maendeleo ya Kariakoo, akisema amekuwa mstari wa mbele kila mara kulinda maslahi ya eneo hilo.
“Zungu ni zaidi ya mzazi kwangu  ni rafiki wa karibu. Kukiwa na shida Kariakoo, hata kama yuko mbali, huwa anapiga simu kushughulikia.” Amesema.
“Ni wakati wa kuchagua maendeleo. Tupige kura kwa Rais Samia, Mussa Zungu, na Haji Manara  kwa pamoja tutaleta mageuzi ya kweli Kariakoo.”
Katika mkutano huo, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameshiriki na kutoa majibu ya moja kwa moja kuhusu changamoto ya maji na maji taka inayoikabili Kariakoo.
Aweso ameeleza kuwa serikali kupitia DAWASA na ufadhili wa zaidi ya Sh. Bilioni 200 kutoka Korea, inaendelea kutekeleza mradi mkubwa wa maboresho ya mfumo wa maji taka katika maeneo ya Kariakoo, Jangwani, Mchikichini na mengineyo.

You Might Also Like

Imarisheni Mkakati Wa Kusimamia Usafi Wa Mazingira-Mhagama

Waomba Kuondolewa Vikwazo Vya Biashara Ya Mazao Ya Kilimo Ikolojia Mipakani

Mkuu wa Mkoa akabidhi matrekta kwa wakulima kutoka Pass Leasing

UDSM Yaanzisha Mkakati Kuokoa Nyuki Wadogo

Tanzania Yanadi Nishati Kimataifa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wananchi Uyui Wafurika Kumsubiri Mgombea Urais CCM
Next Article TEA Yatathmini Utekelezaji na Kupanga Mwelekeo Mpya Kupitia Baraza la Wafanyakazi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Rais Wa CWT Suleiman Ikomba Sasa Ni Daktari
Habari September 13, 2025
Salum Mwalim: Nitarejesha Hadhi ya Kanda ya Ziwa na Kuinua Zao la Pamba
Habari September 12, 2025
TEA Yatathmini Utekelezaji na Kupanga Mwelekeo Mpya Kupitia Baraza la Wafanyakazi
Habari September 12, 2025
Wananchi Uyui Wafurika Kumsubiri Mgombea Urais CCM
Habari September 11, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?