MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Makampuni 408 Ya Tanzania Yaruhusiwa Kusafirisha Mazao Ya Kilimo Kwenda China
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Makampuni 408 Ya Tanzania Yaruhusiwa Kusafirisha Mazao Ya Kilimo Kwenda China
Habari

Makampuni 408 Ya Tanzania Yaruhusiwa Kusafirisha Mazao Ya Kilimo Kwenda China

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imesema kuwa Serikali imefanikiwa kuratibu na kuwezesha usajili wa makampuni 408 ya Kitanzania kuruhusiwa kusafirisha mazao mbalimbali ya kilimo kwenda soko la China.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, mafanikio hayo yamepatikana kupitia ushirikiano kati ya Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ubalozi wa Tanzania nchini China pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Makampuni hayo yamesajiliwa rasmi katika mfumo wa Mamlaka Kuu ya Forodha ya China, huku orodha ya makampuni husika ikiambatanishwa na taarifa hiyo.
TPHPA imeeleza kuwa usajili huo ni sehemu ya utekelezaji wa masharti ya Afya na Usalama wa Mimea na Chakula pamoja na makubaliano ya kibiashara kati ya Tanzania na China.
Lengo ni kuhakikisha kuwa mazao ya kilimo yanayosafirishwa kwenda nchini humo yanakidhi viwango vya afya ya mimea, ubora na usalama wa chakula vinavyotakiwa na soko la China.
Mamlaka imewakumbusha makampuni yote yaliyosajiliwa kuendelea kuzingatia kikamilifu masharti ya usimamizi wa afya ya mimea, ufuatiliaji wa mazao, matumizi sahihi ya viuatilifu pamoja na taratibu zote za ukaguzi kabla ya usafirishaji.
Aidha, TPHPA imetoa wito kwa makampuni mengine yanayopenda kusafirisha mazao ya kilimo kwenda China kuwasilisha maombi yao kupitia Mamlaka hiyo kwa ajili ya kupatiwa mwongozo wa taratibu za kuingia katika soko la China kupitia mfumo wa GACC.
Vilevile, Mamlaka imewahimiza wadau wote wa sekta ya kilimo na biashara kuendelea kushirikiana na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili Tanzania inufaike kikamilifu na fursa kubwa ya soko la China.
Soko hilo linatarajiwa kuongeza mauzo ya mazao ya kilimo nje ya nchi, kukuza uchumi wa wakulima na kuchangia pato la taifa.
TPHPA imesisitiza kuwa itaendelea kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuhakikisha masharti ya kitaifa na ya nchi lengwa yanazingatiwa ipasavyo.
TPHPA imetoa shukrani kwa uongozi wa Wizara ya Kilimo kwa kuiwezesha Mamlaka kufanikisha upatikanaji wa soko la China.
Aidha, Mamlaka imeahidi kuendelea kufungua masoko ya bidhaa za kilimo katika nchi nyingine duniani, ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika utekelezaji wa Ajenda ya 10/30 ya Wizara ya Kilimo.

You Might Also Like

Majaliwa Aomba Watanzania Wapatiwe Mafunzo Belarus Kuendeleza Kilimo

Serikali Kukarabati Vituo Vyote Vya Kutolea Huduma Za Afya Kongwe

Watahiniwa 72 wa kidato cha nne wafutiwa mtihani kwa udanganyifu, kuandika lugha za matusi

BoT Yawaalika Wachimbaji Kuwekeza Serikalini, Yatoa Elimu ya Fedha

TARI Yawafikia Wakulima Kilosa, Kilimo Shadidi Cha Mpunga

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yaweka Utaratibu Biashara Pembezoni mwa Barabara
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Yaweka Utaratibu Biashara Pembezoni mwa Barabara
Habari February 5, 2026
TEHAMA Kuchochea Uchumi wa Kidijitali, Serikali Yatenga Sh Bil Tano Kwa Kampuni Changa
Habari February 5, 2026
Wananchi wa Bukoba Wapewa Vizimba vya Samaki Kuongeza Mapato
Habari February 4, 2026
Serikali Yaanza Mchakato wa Kujenga Uwanja wa Ndege Kyabajwa
Habari February 4, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?