Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Halmashauri ya Manispaa ya Longido iliyopo Arusha, kutenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uzio wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Longido Samia Girls kwa lengo la kuimarisha ulinzi.
Katibu wa Halmashauri Kuu CCM Taifa(NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, ameeleza hayo alipotembelea shule hiyo ya sayansi ya wasichana ya kidato cha tano na sita akiwa katika ziara yake mkoani Arusha.

Makalla amesema ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi hao inapaswa halmashauri hiyo itoe fedha kwa ajili ya kuanzisha msingi wa ujenzi wa uzio, kisha atazungumza na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kwa lengo la kumalizia ujenzi huo.