Na Steven Nyamiti, (REA)
GEITA: WAKALA wa Nishati Vijijini (REA), umesema majiko banifu yanayotolewa kwa bei ya ruzuku yanayotumia kiasi kidogo cha mkaa kulinganisha na majiko mengine ya mkaa.
Wataalam kutoka REA wamesema hayo katika elimu wanayoitoa katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita.

Picha zote zimepigwa na Steven Nyamiti kutoka Wakala wa Nishati Vijijini ( REA)
Kuhusu majiko banifu hayo, wataalam hao wa REA wamesema yametengenezwa kwa teknolojia ya kisasa yenye uwezo wa kupunguza sumu ya mkaa, hivyo inasaidia kupunguza madhara ya kiafya yatokanayo na nishati ya mkaa.
Pia amesema majiko banifu yanasaidia utunzaji wa mazingira, ni rahisi kwa matumizi, yanadumu kwa muda mrefu bila kupata changamoto ya kuharibika kwa watumiaji.
Katika mkoa wa Geita, kampuni inayosambaza majiko banifu kwa bei ya ruzuku ni Geita Millenium Star Company Limited.

Majiko banifu yanatolewa kwa bei ya ruzuku ya Sh.6,195 kwa kuwa Serikali imeweka ruzuku ya bei katika majiko hayo ili wananchi waweze kuyatumia na kuyapata kwa urahisi, ambapo kabla ya ruzuku yalikuwa yanauzwa kwa Sh. 41,300.