Na Lucy Ngowi
DODOMA: ILI wananchi waweze kupata huduma ya barua ya utambulisho inapaswa awe na anuani ya makazi iliyosajiliwa kwenye mfumo wa NaPA.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesena hayo leo Februari nane, 2025 wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Anuani za Makazi yaliyofanyika jijini Dodoma.

Majaliwa amesema mwananchi akiwa na anwani hiyo ya makazi, hatafuata tena huduma ya utambulisho katika Ofisi za Serikali ya kijiji, mtaa ama sheha.
Amesema Rais Samia amewezesha utekelezaji wa mfumo huo wa anwani za makazi nchini kwa njia ya operesheni uliouzindua.
“Hatua hii iliyofikiwa na nchi katika utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi ni ya kujivunia kwani hata nchi jirani ikiwemo za Uganda, Comorro na Eswatini zinaleta wataalamu kujifunza uzoefu “
“
Hii, ni fursa kwa wataalamu wa ndani kutumika kueneza uzoefu kwa mataifa mengine.
Amesisitixa kwamba utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi ni endelevu kwa sababu ya mabadiliko ya makazi na huduma.
Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaendelea kusimamia na kuendeleza miundombinu na mifumo ya msingi, ambayo ni mhimili muhimu wa uchumi wa kidijitali ulioainishwa katika Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali wa Miaka 10 (2024–2034).
Amesema mifumo hiyo inajumuisha mifumo ya utambuzi wa watu, biashara, ardhi, na makazi. “Katika muktadha huu, utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi ni hatua ya kimapinduzi inayolenga kuboresha utambuzi na utoaji wa huduma kwa wananchi hapa nchini.”