.Na Mwandishi Wetu
DODOMA: WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema ifikapo mwishoni mwa Disemba mwaka huu, iwe ni mwisho kwa matumizi ya mkaa na kuni kwa taasisi zinazoandaa chakula kwa zaidi ya watu 100.
Aidha Majaliwa ameshauri matumizi ya teknolojia ya nishati safi ya kupikia,.
Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Novemba 07, 2024 alipotembelea na kukagua hatua za maandalizi ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi za kupikia katika Gereza la Isanga, Dodoma
Katika hilo amesema, Serikali itafanya ukaguzi kwa kila Taasisi kuona utekelezaji wa agizo hilo.
Ameeleza manufaa ya kutumia nishati safi y
Ni pamoja na kutokuwepo na moshi wakati wa utumiaji hivyo kupunguza madhara ya kiafya kwa mtumiaji tofauti na matumizi ya kuni pia teknolojia hiyo inauwezo wa kupika chakula kingi kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameishukuru Serikali kwa kazi inayofanya katika kuleta mabadiliko makubwa kwa Wizara na vyombo vyake vya usalama ikiwemo Jeshi la Magereza.
Masauni amesema Gereza hilo la Isanga limechangamkia fursa ya utekelezaji wa azma ya Serikali kwa vitendo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa nishati safi za kupikia Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Jeremiah Katungu amesema Gereza hilo limeshaanza utekelezaji wa mkakati huo kama ilivyokusudiwa kwa kupokea jumla ya tani 15 za mkaa mbadala na majiko sita na utaratibu wa kusimika mifumo ya matumizi ya gesi ya LPG unaendelea na utakamilika hivi karibuni.