Na Danson Kaijage
DODOMA: Machite Mgulambwa, mdogo wa aliyekuwa Spika wa Bunge, marehemu Job Ndugai, amesema kifo cha kaka yake kimetokea kwa ghafla, akieleza kuwa kilisababishwa na mafua na kifua.
Machite ameeleza kuwa hadi tarehe 4 Agosti 2025, siku ya kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM jimbo la Kongwa, Ndugai alikuwa na afya njema na alihitimisha kampeni zake kwa mafanikio.
Agosti tano, 2025 majira ya asubuhi Machite alizungumza naye kwa simu, ambapo Ndugai alilalamikia hali ya mafua na kifua lakini akasisitiza si tatizo kubwa.
ALimweleza kuwa atapumzika mjini kutokana na uchovu na vumbi la kampeni. Machite pia alieleza kuwa Ndugai alionekana na mipango ya msimu wa kilimo, jambo linaloonesha hakuwa na dalili za ugonjwa mbaya.
Kifo chake kimetangazwa rasmi na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson,