MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: LHRC Kushirikiana  Na JOWUTA Kuwajengea Uwezo Wanahabari Katika Masuala Ya Haki Zao Na Sheria Za Kazi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > LHRC Kushirikiana  Na JOWUTA Kuwajengea Uwezo Wanahabari Katika Masuala Ya Haki Zao Na Sheria Za Kazi
Habari

LHRC Kushirikiana  Na JOWUTA Kuwajengea Uwezo Wanahabari Katika Masuala Ya Haki Zao Na Sheria Za Kazi

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi wetu
DAR ES SALAAM: KITUO  cha Sheria Na Haki Za Binadamu (LHRC),  kimeahidi kufanyakazi na Chama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari (JOWUTA)  katika kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu sheria za kazi na sheria zinazohusu sekta ya habari.
Mkurugenzi wa Uchechemuzi na Maboresho LHRC, Fulgence Massawe  ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na viongozi wa JOWUTA Makao Makuu ya LHRC.
Massawe amesema LHRC ni mdau mkubwa wa wanahabari na tasnia ya habari hivyo wakati wote wapo tayari kufanyakazi na JOWUTA kusaidia kuboresha tasnia ya habari nchini.
“Tunajua changamoto katika sekta ya habari,i kiwepo asilimia zaidi ya 80 ya wanahabari kutokuwa na mikataba wala ajira lakini pia tunajua uchumi mbaya wa vyombo vya habari,” amesema
Amesema uchumi mbaya wa vyombo vya habari sio kigezo cha kushindwa kuheshimiwa sheria za kazi zilizopo nchini.
“Tutashirikiana kutoa elimu kwa wanahabari,waajiri na wadau ili kuona ni jinsi gani waandishi wanafanyakazi kwa kuzingatia maadili lakini wanakuwa na uhuru wa kufanyakazi na katika mazingira bora,” amesema.
Mwenyekiti wa Taifa wa JOWUTA Mussa Juma amemweleza Massawe kwamba, JOWUTA inahitaji ushirikiano na wadau mbalimbali katika kutetea maslahi bora ya waandishi wa habari.
“Bado kuna waajiri wengi hawalipi wanahabari na wala hawatoi mikataba jambo ambalo ni kinyume cha sheria za kazi hivyo JOWUTA itaendelea kupigania haki za wanahabari ikiwepo mazingira bora ya kazi,” amesema.
Amesema tayari JOWUTA imesaidia baadhi ya wanahabari kwenda mahakamani kudai stahiki zao lakini bado changamoto ni kubwa.
“Tumekuja hapa kujadiliana juu ya ushirikiano wetu lakini pia kama viongozi wapya wa JOWUTA kujitambulisha kwa wadau,” amesema.
Juma ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Shirikisho la Waandishi wa Habari Afrika Mashariki na Kati, ametaka LHRC kufanya kazi na JOWUTA hasa kuelekea katika chaguzi ambapo wanahabari wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi.
Naye Katibu Mkuu wa JOWUTA Seleman Msuya amesema JOWUTA ndio chama pekee kisheria nchini chenye jukumu la kulinda na kutetea maslahi bora ya kazi kwa waandishi na mazingira bora ya kazi.
“Sisi ndio tunaweza kuwapeleka waajiri mahakamani na tunafanya hivyo lakini bado changamoto ni nyingi ndio sababu tunaomba ushirikiano na wadau wakiwepo LHRC,”amesema.
Katika ziara hiyo pia mweka hazina wa JOWUTA Lucy Ngowi amesema  kutokana na hali ngumu za kimaisha kwa waandishi wengi hata uchangiaji wa ada za chama imekuwa ni tatizo.
Viongozi wa JOWUTA bado wanaendelea na ziara kwa wadau mbalimbali kuelekea uzinduzi wa mafunzo ya wanahabari kuhusiana na kuripoti vyema uchaguzi mkuu lakini wakiwa salama  ikiwepo kutonyanyaswa na vyombo vya dola ama vyama vya siasa.
.

You Might Also Like

TEA, Wadau Kuwezesha Matumizi Safi Nishati Ya Kupikia Mashuleni

Imarisheni Mkakati Wa Kusimamia Usafi Wa Mazingira-Mhagama

Ridhiwani: Maandalizi Mei Mosi  Yafikia Asilimia 88

Mtafiti UDSM Atafiti Mimea Ya Asili Kudhiti Fangasi Kwenye Mimea

Makala: Hakuna Kupita Bila Kupingwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Waziri Mkuu Majaliwa Ahimiza Watanzania Kufanya Mazoezi
Next Article TPHPA, KEM Wasaini Hati Ya Makubaliano Udhibiti Viuatilifu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?