MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kongamano  La Kimataifa La Jotoardhi Laanza Kwa Mafanikio
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kongamano  La Kimataifa La Jotoardhi Laanza Kwa Mafanikio
Habari

Kongamano  La Kimataifa La Jotoardhi Laanza Kwa Mafanikio

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
KONGAMANO  la 10 la Jotoardhi Afrika (ARGeo-C10) limeanza kwa mafanikio jijini Dar es Salaam ambapo Wataalam takriban 800 kutoka 21 duniani wameshiriki.
Hayo yameelezwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Innocent Luoga wakati akifungua mafunzo kuhusu masuala mbalimbali ya Jotoardhi kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu ikiwa ni sehemu ya programu ya siku saba za kongamano hilo.
“Katika Kongamano hili washiriki watafaidika na masuala mbalimbali ikiwemo kupata ufahamu wa kina kuhusu maendeleo ya rasilimali za jotoardhi kupitia mazungumzo na warsha za kiufundi, Kubadilishana uzoefu, kutembelea na kujifunza kwa vitendo katika maeneo ya miradi ya jotoardhi, kujadili athari za masoko ya kaboni na kukuza uwezo kupitia kozi fupi za kiufundii” amesema  Luoga.
Ameongeza kuwa, Tanzania imekuwa mwenyeji wa kongamano hilo kutokana na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uendelezaji wa Sekta ya Nishati ikiwemo jotoardhi.
“ Ili tuweze kuwa na umeme wa uhakika na usalama wa nishati nchini lazima umeme uzalishwe kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo maji, gesi, jua, upepo na jotoardhi yenyewe na lengo la Serikali ni kuachana na utegemezi vyanzo vichache vya umeme.” amesema Luoga
Ametanabaisha kuwa, Tanzania ina maeneo takriban 52 yaliyoainishwa kwa ajili ya uendelezaji wa  nishati ya jotoardhi ambapo maeneo matano tayari yanaendelezwa, ikiwemo Ngozi, Kiejo-Mbaka, Ruhoi, Natron na Songwe.
Ameeleza kuwa, kongamano hilo la Kimataifa la Jotoardhi linaamsha ari mpya katika uendelezaji wa jotoardhi Tanzania kwani litasaidia pia kuongeza fursa za uwekezaji kwenye sekta hiyo.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mathew Mwangomba amesema kongamano hilo linahusisha wadau mbalimbali duniani ikiwemo watalam wa jotoardhi ambao wataangazia masuala mbalimbali ikiwemo masoko ya gesi ya ukaa na upunguzaji wa gesi ya ukaa.
Ametaja Kauli mbiu ya Kongamano hilo kuwa ni, Kuharakisha Maendeleo ya Rasilimali za Jotoardhi katika Afrika, masoko ya gesi ya ukaa na upunguzaji wa gesi ya ukaa.
Ametaja faida za ARGeo- C10 kuwa ni pamoja na kufungua fursa zinazotokana na jotoardhi na kuharakisha maendeleo ya nishati hiyo Tazania hali itakayoongeza pia pato la Taifa na kuongeza kiasi cha umeme.
Amesema Kongamano kama hilo  lilifanyika mwaka 2014 nchini Tanzania na kuleta matokeo chanya ikiwemo uanzishwaji wa kampuni ya Jotoardhi Tanzania, Wataalam wa Kitanzania kupata mafunzo nje ya nchi na kuongeza mchango wa wadau wa maendeleo katika jotoardhi ikiwemo Japan (JICA), Iceland, New Zealand na Marekani.
Naye, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maziringira (UNEP) katika nchi za Kusini mwa Afrika, Meseret Teklemarian ameipongeza Tanzania kwa kuandaa kongamano hilo kwa mafanikio makubwa.

You Might Also Like

Rais Samia azindua bwawa la umwagiliaji Mtibwa

Japan Yatoa Bilioni 27 Kuboresha Sekta Ya Afya

TANESCO Tunathamini Wadau Wa Maendeleo- Nyamo-Hanga

Kaguo Ataja Mbinu Mpya Ukwepaji Kodi Kwenye Mafuta

TFS Yawataka Wananchi Kufuga Nyuki Kuzuia Uharibifu Wa Mazingira

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Biteko Akaribisha Wawekezaji Sekta Ya Nishati
Next Article Sababu Nne Zilizofanikisha Mafanikio Katika Uandikishaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?