MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kiwanda cha Sukari Mkulazi Chaanza Kuleta Tija, Sangu Apongeza Uwekezaji wa NSSF na Magereza
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kiwanda cha Sukari Mkulazi Chaanza Kuleta Tija, Sangu Apongeza Uwekezaji wa NSSF na Magereza
Habari

Kiwanda cha Sukari Mkulazi Chaanza Kuleta Tija, Sangu Apongeza Uwekezaji wa NSSF na Magereza

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
4 Min Read
Na Mwandishi Wetu
MOROGORO: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, ameridhishwa na hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa katika mradi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi, akisema kuwa ndani ya muda mfupi kiwanda hicho kitaanza kujiendesha kwa faida.
Hatua hiyo inaendana na maono ya Serikali ya kuridhia kuendelea kwa mradi huo wa kimkakati.
Sangu ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya mradi huo, akiwa ameambatana na wabia wa kiwanda hicho, akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, pamoja na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, ACP Dominic Kazmil.
Habari Picha 10908
Kiwanda hicho kinamilikiwa kwa ubia kati ya NSSF na Jeshi la Magereza kupitia Shirika la Uzalishaji Mali (SHIMA).
“Niwapongeze sana wawekezaji wa mradi huu, NSSF na Jeshi la Magereza. Kama Serikali, tunashukuru kwa mchango mkubwa wa mradi huu katika kuzalisha ajira, jambo ambalo ndilo muelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,” amesema Sangu.
Amebainisha kuwa mradi huo tayari umeanza kuleta tija kwa Taifa na jamii kwa ujumla, ambapo hadi sasa umefanikiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,920 na ajira zisizo za moja kwa moja takribani 8,000 ndani ya muda mfupi tangu ulipoanza kutekelezwa.
Sangu amesema manufaa ya kiwanda hicho ni pamoja na kuchochea uchumi wa nchi, kuongeza mapato ya kodi, kuzalisha ajira kwa Watanzania na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, hususan kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho.
“Kiwanda hiki ni cha kimkakati na kinatekeleza maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuacha tabasamu kwa Watanzania, kwani tayari mradi huu umeanza kuleta mabadiliko makubwa kwa Taifa na jamii kwa ujumla,” amesema.
Aidha, amepongeza Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara zinazounganisha mashamba ya wakulima wadogo wa miwa na kiwandani, hatua inayorahisisha usafirishaji wa miwa kutoka mashambani hadi kiwandani.
Ameahidi kuufuatilia mradi huo kwa karibu ili kuhakikisha unatimiza lengo la kupunguza nakisi ya sukari nchini, akieleza kuwa katika mwaka wa uzalishaji 2027/2028, kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha tani 50,000 za sukari.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni Hodhi ya Mkulazi, Dkt. Hildelitha Msita, ameishukuru Serikali kwa kuwekeza katika miradi inayogusa maisha ya wananchi na kukuza uchumi, huku akiahidi kuendelea kuusimamia mradi huo kwa weledi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ameishukuru Serikali kwa usimamizi mzuri wa mradi huo, akibainisha kuwa wabia watahakikisha kiwanda kinasimamiwa ipasavyo ili malengo ya mradi yatimie na kuleta faida endelevu kwa wanachama na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, ACP Kazmil amesisitiza kuwa ushirikiano uliopo kati ya NSSF na Jeshi la Magereza umechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya mradi huo.
Diwani wa Kata ya Mkulazi, Edward William, ameishukuru Serikali kwa uwekezaji wa kiwanda hicho, akisema kuwa kimeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa kata hiyo kupitia ajira, fursa za kiuchumi na uboreshaji wa huduma za kijamii.
Habari Picha 10909
Habari Picha 10910
Habari Picha 10911
Habari Picha 10912
Habari Picha 10913
Habari Picha 10914
Habari Picha 10915
Habari Picha 10916
Habari Picha 10917
Habari Picha 10918
Habari Picha 10919
Habari Picha 10920
Habari Picha 10921
Habari Picha 10922
Habari Picha 10923
Habari Picha 10924
Habari Picha 10925

You Might Also Like

Rais Mpya CWT Ikomba: ‘Nataka Kuwaunganisha Walimu, Kuitendea Haki Kazi Yetu’

Gridi Ya Taifa Ni Dhaifu Kwa Mikoa Ya Kaskazini-Mramba

Waziri wa Vijana akutana na Mwita wa Zanzibar

Biashara Kati Ya Tanzania Na Uturuki Yapanuka Kwa Kiasi  Kikubwa

Viongozi Wa Dini Zote Wajifungie Kuomba,Kujadili Na Kutoa Mapendekezo-SAU

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tril.1.5/- Za Umeme Vitongojini: Ndejembi Awasihi Ma-RC Na DC Kusimamia Kwa Ufanisi Mradi
Next Article Bil 67 Zatumika Kujenga Barabara, Masoko  Mwanza-Profesa Shemdoe
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?