Na Lucy Lyatuu, Singida
KATIKA maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza neema kwa wafanyakazi wa serikali kwamba kuanzia Julai 2025 mshahara utaongezeka kwa asilimia 35.1 na kuwezesha wafanyakazi wa kima cha chini kulipwa shilingi 500,000 kutoka 370,000 ya sasa.
Akizungumza katika madhimisho ya Mei Mosi mwaka huu, Rais Samia ametangaza nyongeza hiyo ya mishahara ya kima cha chini kwa asilimia 35.1 kwa wafanyakazi wa serikali ambapo watakuwa wanalipwa mishahara wa sh 500,000 kutoka sh 370 ,000 kuanzia Julai mosi 2025.
Amesema kwa sekta binafsi mchakato wa nyongeza unaendelea kupitia bodi ya mishahara ya sekta binafsi.
Rais Samia amesema.serikali imefikia uamuzi huo.baada ya uchumi kuanza kuimarika kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji nchini.
Amesema uchumi kwa sasa umefikia asilimia 5.5 kutoka 4.6 mwaka 2024, hivyo anaona ni wakati muafaka wa kuongeza mshahara.
Tangazo hilo la Rais lilipokewa kwa shangwe na nderemo na maelfu ya wafanyanyakazi waliokuwa wamejitokeza anbao swali walionekana kupoa kiwanjani hapo.
Kwa upande wake Waziri wa Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema atahakikisha utatu unasimamiwa katika wizara yake ili kila upande uweze kunufaika.
Kuhusu vyama vya wafanyakazi Rais Samia amevitaka viwe chachu ya maendeleo na kuzingatia sheria za kazi ambao wanaosimamia.