Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, amekutana na Katibu Mkuu wa Chama tawala nchini Comoro cha Convention for the Renewal of the Comoros (CRC), Youssoufa Mohamed Ali, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya vyama hivyo.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Youssoufa Mohamed Ali,pia ni Waziri wa Ulinzi na Katibu wa Rais wa Comoro, yupo nchini kwa ziara ya kikazi iliyoanza Novemba mbili hadi tano, 2024.