Na Mwandishi Wetu
ASKOFU wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Mashariki Kati Kusini, Dkt. Lawrence Kametta, amewataka watanzania kukataa kununuliwa katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu 2025.
Amesema katika uchaguzi wa Serikali ya mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025, watanzania wawe makini katika kuchagua viongozi waadilifu na watenda haki pia
Wito huo ameuroa jijini Dar es Salaam alipoalikwa kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 13 ya Moto wa Uamsho ya Chuo cha Kupanda Makanisa (CCKM),ambapo alisema ni jukumu la viongozi wa Dini ,wananchi kuombea taifa liwe na amani hasa katika kipindi cha uchaguzi.

Ameesema ili kila mtanzania aweze apige kura
na kumchagua kiongozi anayefaa ni vyema kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate haki hiyo.
Aliwataka watanzania kua makini wasikubali kununuliwa kila mmoja ashiriki na ashinde kwa haki.
“Tuombee uchaguzi tuombee amani,watu wajitokeze kwa wingi kuhakiki majina yao ili wapate nafasi kuchagua viongozi watakaofaa na kumcha Mungu pia na wenye kuwajibika ipasavyo katika nafasi hizo,”
“Pia tumuombee Rais Samia apewe hekima na maarifa na pia kuwaombea wasaidizi na washauri wake wawe wanampa taarifa nzuri zilizochujwa ili kuwe na maamuzi sahihi pia,”amesema.

Amewataka waumini wa dini mbalimbali kutohofia kugombea kwani viongozi wakiwa wachaMungu pia taifa linakua lenye amani siku zote.
“Msiache watu wasio na hofu ya Mungu wakaongoza nchi. Tuombe amani na haki itendeke, wabunge wasimame kwa uadilifu, na mahakama isiingiliwe na wala rushwa,” aesema.
Katika hafla hiyo, wanafunzi 50 walihitimu mafunzo ya awali ya uinjilisti, ikionyesha jitihada za kuendeleza injili na utumishi wa kanisa.
Mwisho