Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imesema Mamlaka ya Elimu Tanzania ( TEA), inafanya kazi kubwa katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Florence Kyombo amesema hayo Leo Februari 19, 2025 katika ziara ya kikazi Kisiwani Unguja Zanzibar.
Kyombo amesema miradi hiyo ya TEA imekuwa na manufaa kwa jamii.

“TEA inafanya kazi kubwa sana kwenye uboreshaji wa miundombinu ya elimu kote nchini sioZanzibar pekee.
“Ukipita maeneo ya vijijini na pembezoni mwa mji, utaiona miradi yao mingi ambayo inaendelea kutatua changamoto za miundombinu ya elimu,”amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi zmkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano 2019/2020 hadi2024/ 2025 mamlaka hiyo imetekeleza miradi yenye thamani ya Sh. Bilioni 2.8.

Amesema kati ya kiasi hicho Sh. Bilioni 2.1 zimeboresha miundombinu ya elimu, Sh. Milioni 574.3 zimeelekezwa kufadhili mafunzo ya kuendeleza ujuzi (SDF) kwa vijana 600 kutoka kaya maskini.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Dkt. Leonard Akwilapo ameshukuru kamati hiyo, kwa kutambua juhudi za mamlaka na kuahidi kusimamia kwa weledi utekelezaji wa miradi yote ya elimu Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutafuta rasilimali fedha ili kufadhili miradi mingi zaidi kwa maendeleo ya sekta ya elimu.