Na Lucy Ngowi
PWANI: KAMATI ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, imeipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa uzalishaji wa chanjo za mifugo ambazo zinatumika kuboresha afya za mifugo hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deodatus Mwanyika kwa niaba ya kamati nzima iliipotembelea Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Naye Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema mipango ya Wizara ni kuendelea kuhamasisha pamoja na kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu umuhimu wa kuchanja mifugo

Kwa upande Wake, Mtendaji Mkuu wa TVLA, Dkt. Stella Bitanyi amesema kwa sasa wameanza kuwafikia wafugaji moja kwa moja kuwapa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa mifugo yao.

Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) ipo chini ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ambapo jukumu lake kubwa ni kufanya tafiti na kuzalisha chanjo.
