Na Lucy Lyatuu
JESHI la Polisi,Kanda Maaalum Ya Dar es Salaam limesema itaimarisha ulinzi kwa siku mbili katika jiji hilo wakati wa mchezo kati ya timu mbili za Simba dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini na timu ya Yanga na Silver strikers ya Malawi.
Kamanda wa Polisi wa Kamda Maalum ya Dar es Salaam, JUmanne Muliro amesema timu hizo zinatarajiwa kucheza kuanzia kesho na keshokutwa katika uwanja wa Taifa ikiw ani mchezo wa marudio baada ya timu hizo kucheza mchezo wa awali.
Akizungumza amesema mechi hizo zinachezwa ikiwa kampeni zinaendelea na Jeshi hilo litafanya ukaguzi maalum kwa mashabiki wakatakaoingia katika uwanja huo wakitakiwa kutokuwa na aina yoyote ya siliha inayoweza kumuumiza mtu.
Kuhusu timu ya Yanga amesema mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kuanza saa 11;00 jioni na Simba ikicheza Jumapili kuanzia saa 10:00 jioni ambapo Jeshi hilo linaamini kutakuwa na mkusanyiko mkubwa wa idadi ya mashabiki watakaokwenda uwanjani.
“Mchezo unakusanya hizia tofauti na unatarajia kukusanya watu wengi na uwanja una uwezo wa kuhudumia watu zaidi ya 60,000 na jeshi hilo linahitaji kuona kila anayeingia anatoka salama,”amesema.
Amesema bila kujali aina ya matokeo katika michezo hiyo ni lazima watu watoke salama na kwamba Jeshi hilo linawatahadharisha kuwa litaimarisha mifumo ya usalama.
Amesema ukaguzi wa hali ya juu utafanyika kwa michezo yote na kwamba haitakiwi kuwana kitu chochote kinachoweza kusababisha madhara na kwamba barabara inayopitia Chuo Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) itafungwa.
Amesema ni muhimu mashabiki kuwa wastaarabu kwa kuwa soko ni burudani na kwamba kusiwe na aina yoyote ya matusi na ayakayebainika ataaibishwa na Jeshi hilo

