Na Lucy Lyatuu
BODI ya Ithibati Ya Waandishi Wa Habari (JAB) imeanza rasmi kutoa kitambulisho maalum kwa wanataaluma hiyo hatua inayolenga kuimarisha usimamizi wa taaluma ya uandishi wa Habari.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Tido Mhando amesema hay oleo Dar es Salaam na kuongeza kuwa vitambulisho hivyo vitapatikana kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa TAI-Habari.
Akizungumza amesema Bodi hiyo kuanza kutoa vitambulisho kwa waandishi wa Habari inasaidia kuwatambua rasmi na kuwasajili jambo linaloonesha kuwa watakuwa na uhalali na kurahisisha huduma nauhakiki kwa wanataaluma hao.
Amesema ili kupata kitambulisho hicho mwandishi wa habari peke yake ndiye anayestahili kutuma maombi yake kupitia mfumo huo ambao ni https//taihabari.jab.gotz na kufuata maelekezo.
Aidha amesema ilikujisajili katika mfumo huo mwombaji anapaswa kuwa namba ya sim una barua pepe vinavyofanya kazi,picha ndogo iliyoskaniwa,vyeti vya elimu vilivyoskaniwa, barua ya utambulisho kutoka taasisi anayotoka au anakopeleka kazi zake ikiw ani mwandishi wa kujitegemea.
Amesema mahitaji mengine anayopaswa kuwa nayo mwombaji ni nakala ya kitambulisho cha Taif ana ada ya ithibati sh 50,000.
Mhando amesema yapo mambo yakuzingatia wakati wa kutuma maombi ambayo ni Pamoja nav yeti kuwa halali na vilivyohakikiwa na mamlaka husika, taarifa ziwe sahihi kuepusha usumbufu na picha iwe ya hivi karibuni.
Amesema kitambusho cha JAB kinaweza kutumika mahali popote ambapo shughuli za kihabari zinafanyika na mahali popote ambapo mwandishi wa Habari anataka kufanya kazi ya kutafuta Habari isipokuwa maeneo maalum yaliyozuiliwa kisheria.
Kuhusu uhalali wa kitambulisho hicho amesema kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari sura 229 inayounda Bodi hiyo aliyethibitishwa atapewa kitambulisho ambacho kitakuwa ndio uthibitisho.
Amesema atakayepewa kitambulisho ni mwandishi wa Habari halali aliyethibitishwa kwa kipindi kilichoainishwa katika kanuni cha miaka miwili, mmiliki wa kitambulisho anaweza kuomba kwa Bodi kuhuisha kitambulisho chake baada ya muda kuisha na mmiliki atalipia malipo yaliyoainishwa.